Askari wanyamapori wa shirika la taasisi ya Grumeti wakiwa katika doria yao ya kawaida karibu la eneo la hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania./Picha: Grumeti Fund

Na Edward Qorro

TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Jumla ya askari wanyamapori 42 barani Afrika wamepoteza maisha katika harakati zao kuhifadhi na kulinda maliasili, kulingana na Shirikisho la Askari Wanyamapori duniani (IRF).

Kwa mujibu wa takwimu za taasisi hiyo, askari hao waliuwawa kati ya kipindi cha Juni 2023 na Mei 2024.

Jumla ya askari wanyamapori 140 kutoka nchi 37 wamepoteza maisha yao wakiwa katika doria zao za kawaida, kulingana na IRF.

“Hii sio taswira halisi ya ulimweguni kwani ilikuwa vigumu kupata taarifa kutoka baadhi ya nchi”.

“Hata hivyo, tunatambua baadhi ya askari waliojitolea uhai wao kulinda rasilimali ulimwenguni," limesema shirika hilo.

Jumla ya askari wanyamapori 140 kutoka nchi 37 wamepoteza maisha yao wakiwa katika doria zao za kawaida, kulingana na IRF./Picha: Getty

Hata hivyo, bara la Asia, ndilo linaloongoza kwa vifo vingi, likiripoti matukio 74, huku mabara ya Ulaya na Amerika Kusini yanashika nafasi ya tatu, yakiwa na vifo sita, mtawalia.

Ni askari mmoja tu aliyeuwawa Amerika ya Kaskazini wakati bara la Australia halikuwa na kifo chochote katika kipindi hicho tajwa, kulingana na IRF.

Jumla ya askari wanyamapori 42 barani Afrika wamepoteza maisha katika harakati zao kuhifadhi na kulinda maliasili, kulingana na Shirikisho la Askari Wanyamapori duniani (IRF)./Picha: Grumeti Fund

Takwimu hizo zinakuja wakati dunia inaadhimisha siku ya askari wanyamapori ulimwenguni, katika kutambua na kuthamini mchango wao katika uhifadhi wa mazingira na maliasili.

TRT Afrika