Chama cha upinzani ACT Wazalendo nchini Tanzania Jumapili kimetoa wito kwa kwa mpinzani mwenza CHADEMA kuhairisha maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika Jumatatu jjijini Daresalaam.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X iliyosainiwa na Dorothy Manka, kiongozi wa chama, ACT Wazalendo ilisema kuwa ni wazi kuwa nchi imeingia kwenye mvutano ambao hauna afya kwa mustakbali wa umoja, amani na demokrasia ya nchi.
''Tunatoa wito kwa pande zote kutuliza vichwa na kutoa nafasi kwa hekima na busara za uongozi ili zitumike upata ufumbuzi na suluhisho muafaka,'' ilisema taarifa hiyo.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa muda mfupi baadaye, kutoka kwa CHADEMA inasisitiza kuwa wataendelea na mpango wao wa kuandamana kama ilivyotangazwa mapema.
“Ndugu zangu, Watanzania wenzangu ni kwa msingi huu basi na baada ya mashauriano na viongozi wenzangu nipende kuwatangazia kutakuwa na maandamano kwanzia saa 3 kamili asubuhi, ikumbukwe maandamano yetu ni ya maombolezo na Amani” Amesema Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema.
Matakwa ya Chadema
Chadema iliitisha maandamano kufanyika jijini Daresalaam kutokana na kile walichodai kuwa utumiaji nguvu na ukosefu wa kufuata sheria miongoni mwa vyombo vya usalama.
Chadema imeitaka serikali ya nchi hiyo kupitia Jeshi la Polisi Tanzania kuwarejesha viongozi wake ambao inadai wametekwa na hawajulikani walipo, licha ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa amri kwa Jeshi hilo kuwatafuta.
Serikali imeharamisha maandamano
Wakati huo huo, magari ya Kikosi cha Kutulia Ghasia cha Jeshi la Polisi Tanzania, maarufu kama FFU yalionekana yakizunguka maeneo tofauti ya jiji hilo la kibiashara nchini Tanzania kama dalili za kuimarishwa usalama mbele y amaandamano hayo.
Jeshi la polisi lilitangaza kuwa maandamano hayo ni kinyume cha sheria na kukataa kutoa leseni licha ya ombi la Chadema lililowasilishwa mapema.
''Tunmawaomba Chadema kuahirisha maandamano yao ya tarehe 23 Septemba na pia tunaiomba serikali na polisi kuchukua hatua za kupunguza joto na kutuliza hali ili kujenga mazingira ya mazungumzo ya dhati yanayolenga kupata ufumbuzi sahihi ya mambo yote nayaolalamikiwa napande zote,'' iliendelea kusmea ACT Wazalendo katik ataarifa yao.