Miongo kadhaa ya mzozo kati ya jeshi na makundi mengi ya waasi yameyumbisha mashariki mwa Kongo na kuchochea mgogoro wa kibinadamu wa muda mrefu./ Picha : Reuters 

Watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa kunid la kidini waliwauwa takriban raia 10 katika shambulio la siku ya Ijumaa karibu na mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mamlaka za mitaa na chanzo cha Umoja wa Mataifa kilisema.

Washambuliaji waliwafyatulia watu risasi wanaofanya kazi katika mashamba katika wilaya ya Mulekera nje ya Beni, Meya wa Mulekera Ngongo Mayanga alisema Jumamosi.

Shahidi mmoja wa shambulio alisema alikuwa akifanya kazi shambani aliposikia milio ya risasi muda mfupi baada ya kutengana na binti-mkwe wake.

“Mkwe wangu alikimbili anjia tofauti, lakini kwa bahati mbaya ndipo alipouawa,” alisema, akielezea jinsi alivyokimbilia msituni na kulala huko kwa hofu ya washambuliaji.

Miili saba imekusanywa hadi sasa, ikiwa ni pamoja na ya wanawake watatu, na wahasiriwa wengine watano wameripotiwa mahali pengine, alisema Meya Mayanga.

“Hakika kuna vyombo vingine ambavyo tutavipata huku msako ukiendelea,” alisema kwa njia ya simu na kulaumu kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF).

Makundi ya waasi yahujumu usalama

Chanzo katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Kongo kilisema watu 10 waliuawa.

ADF wanatokea nchi jirani ya Uganda, ambako inaaminiwa kuwa na makao yake mashariki mwa Congo, na imeahidi utiifu kwa Daesh na huendeleza mashambulizi ya mara kwa mara, na kuzidi kuyumbisha eneo ambalo makundi mengi ya wanamgambo yanafanya harakati.

Miongo kadhaa ya mzozo kati ya jeshi na makundi mengi ya waasi yameyumbisha mashariki mwa Kongo na kuchochea mgogoro wa kibinadamu wa muda mrefu.

Mashambulizi yameongezeka katika mwaka uliopita na idadi ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo ilifikia milioni 7.1 mwishoni mwa Machi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kibinadamu la OCHA.

TRT Afrika na mashirika ya habari