Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema amewasili Uturuki kwa mazungumzo na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuhusu mabadilishano ya wafungwa na masuala mengine.
"Ziara rasmi pamoja na mke wangu kuelekea Uturuki . Tutkutana na Rais Erdogan na Mke wa Rais Emine Erdogan," Zelenskyy alisema kupitia akaunti yake ya Telegram siku ya Jumatatu.
Hapo awali, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun alisema kwenye mtandao wa X, "Rais wetu, Bw. Recep Tayyip Erdogan, atakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, ambaye atakuwa akifanya ziara rasmi nchini mwetu kwa mwaliko wa rais wetu, Jumanne, Februari 18, katika Ikulu ya Rais."
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili ushirikiano wa kimkakati wa Uturuki na Ukraine, kwa kuzingatia "kupitia mahusiano katika nyanja zote" na "kushughulikia hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili."
Ziara hiyo pia itatoa nafasi ya "kujadiliana yanayoendelea hivi karibuni nchini Ukraine" na "maswala mengine ya kikanda na kimataifa."
Ziara hiyo imekuja huku maafisa wa Marekani na Urusi wakijiandaa kwa mazungumzo ya ngazi ya juu nchini Saudi Arabia bila ya uwepo wa Kiev.