Erdogan alisisitiza kuwa katika ukanda uliokumbwa na vita, migogoro na mivutano, ushirikiano wa nchi tatu utachangia tu sio tu amani ya kikanda, bali ulimwengu mzima kwa ujumla. /Picha: AA  

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na Waziri Mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif kwenye mkutano wa 24 wa ushirikiano wa Shanghai katika jiji la Astana nchini Kazakhstan.

Wakati wa mkutano wa nchi hizo tatu, viongozi hao walijadili masuala ya kikanda na kimataifa pamoja na maeneo yanayowezekana ya ushirikiano kati ya nchi zao, kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Kuchangia kwenye amani

Rais Erdogan alisisitiza hatua nyingi za pamoja ambazo Uturuki, Azerbaijan na Pakistan zinaweza kuchukua katika nyanja mbalimbali, ambazo alisema zitanufaisha mataifa yote matatu, ilisema taarifa hiyo.

Alisisitiza kuwa katika ukanda uliokumbwa na vita, migogoro na mivutano, ushirikiano wa namna hiyo utachangia sio tu amani ya kikanda, bali ya ulimwengu mzima.

Mkutano huo, ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Uturuki Hakan Fidan, Waziri wa Nishati na Maliasili Alparslan Bayraktar, Waziri wa Fedha na Hazina Mehmet Simsek, Waziri wa Biashara Omer Bolat na mshauri mkuu wa Rais wa Mambo ya Nje na Usalama , Balozi Akif Cagatay Kilic.

TRT Afrika