Vikosi vya usalama vya nchini Uturuki vimewakata makali magaidi wa nne wa kikundi cha PKK, kaskazini mwa Iraq, na wengine wanne wa PKK kusini mashariki kwa Uturuki katika jimbo la Sirnak.
Magaidi hao waligundulika katika mkoa wa Qandil kaskazini mwa Iraq na walikatwa makali kwa shambulio la angani, imesema Wizara ya Ulinzi katika taarifa yake ya Ijumaa.
Wizara hiyo pia imesisitiza kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yataendelea bila kasoro yoyote, ikisema: "Hakuna namna ya kukimbia kwa magaidi, hakuna sehemu salama kwao."
Mara nyingi, magaidi hao hujificha kaskazini mwa Iraq, ng'ambo ya mpaka na Uturuki, wanapopanga mashambulizi yao dhidi ya Uturuki.
Zaidi ya watu 40,000 wauwawa
Katika hatua nyingine, katika operesheni iliyoongozwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki siku ya Ijumaa, majeshi ya nchi hiyo yamefanikiwa kuwakata makali magaidi wanne wa PKK katika eneo la wilaya ya Beytussebap katika jimbo la Sirnak.
Waliokatwa makali katika operesheni ya Bozdogan-44 walikuwa ni gaidi mmoja kutoka orodha ya rangi ya chungwa, na wawili wa rangi ya kijivu. Uturuki hutumia rangi kama kigezo cha kuwatambua magaidi wanaotafutwa, ambapo nyekundu huwakilisha wenye kutafutwa sana, ikifuatiwa na bluu, kijani, machungwa na kijivu.
Akiangazia nia ya Ankara ya kupambana na ugaidi, Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya aliandika kwenye ukurasa wake wa X: ”Tutawaondoa watu hawa dhalimu na wasaliti kutoka kwenye ardhi yetu. Tutawakata hewa zao, mmoja baada ya mmoja.”
Katika miaka yake 40 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, kikundi cha PKK, kimeorodheshwa kama kikundi cha kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, kikihusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000 wakiwemo wanawake na watoto.