Uturuki, Ugiriki wafanya mazungumzo kuhusu hatua za kujenga imani

Uturuki, Ugiriki wafanya mazungumzo kuhusu hatua za kujenga imani

Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema kuwa mkutano huo ulifanyika kwa mtazamo chanya.
Wizara ya Ulinzi ya Ugiriki iliandaa mkutano huo./ Picha: Twitter/@tcsavunma

Wajumbe kutoka Uturuki na Ugiriki wamefanya duru mpya ya mazungumzo kuhusu hatua za kujenga imani, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya Uturuki imetangaza.

Wizara ya Ulinzi ya Ugiriki iliandaa mkutano huo siku ya Jumatatu.

"Ujumbe wa p ande mbili ulijumuisha mabalozi, maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi, pamoja na maafisa wengine," wizara ya Uturuki ilisema kwenye X.

Pande hizo mbili zilipitia hatua zilizokubaliwa hapo awali katika mwaka unaoendelea, na kujadili mpango wa utekelezaji wa 2025, taarifa hiyo ilisema, na kuongeza: "Mkutano ulifanyika kwa mtazamo chanya. Mkutano unaofuata utaandaliwa na upande wa Uturuki."

Mahusiano ya Kirafiki, Ujirani Mwema

Mnamo Desemba 2023, wakati wa ziara ya Erdogan huko Athene, mataifa hayo mawili yalitia saini Azimio la Athens kuhusu Mahusiano ya Kirafiki na Ujirani Mwema.

Tamko hilo lilisisitiza haja ya kuendeleza juhudi za kuboresha mahusiano kwa manufaa ya jamii zote mbili katika mazingira ya urafiki na kuaminiana.

Kutokana na hali hii, walikubali kushiriki katika mashauriano endelevu yenye kujenga na ya maana kwa kuzingatia mazungumzo ya kisiasa, ajenda chanya na hatua za kujenga imani, na kujiepusha na vitendo na kauli ambazo zinaweza kudhoofisha ari ya tamko.

TRT World