Ufanisi wa Uturuki katika ndege zisizokuwa na rubani ni muhimu kwa maendeleo yake ya kijeshi. /Picha: AA

Uturuki itaunda mradi wake wa mfumo wa ulinzi wa anga wa "Steel Dome", rais wa nchi hiyo alisema Jumamosi.

"Tunatumai, tutatekeleza mradi wetu wa 'Steel Dome' pamoja na vijenzi vyake vyote. Ikiwa (Israeli) wako na "Iron Dome", tutakuwa na Steel Dome," Recep Tayyip Erdogan alisema katika Shereha ya Uzinduzi wa Mahafali na Kukabidhi Bendera katika Chuo cha Vita vya Anga.

"Mfumo wa Steel Dome itahakikisha kuwa mifumo yetu ya ulinzi wa anga, vihisi na silaha zote zinafanya kazi kwa ushirikiano," Erdogan alisema.

Erdogan alisisitiza kukua kwa umaarufu wa Uturuki katika teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani.

“Ufanisi wetu katika ndege zisizokuwa na rubani unatazamwa kwa wivu sio tu na mataifa ya kirafiki na udugu bali duniani kote,” alisema.

Kwa kuzinduliwa kwa ndege za Kizilelma na ANKA-3 zisizo na rubani, ambazo majaribio yake yanaendelea, Uturuki itachukua nafasi kubwa katika "ligi mpya" ya sekta hiyo, Erdogan aliongeza.

Kupambana na ugaidi

Rais wa Uturuki pia alisisitiza dhamira ya Uturuki ya kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, akisema: "Tunajitahidi kutengeneza, kuendeleza, au kununua chochote kinachohitajika na Jeshi letu la Anga, kutoka kwa makombora hadi mifumo ya ulinzi wa anga."

"Jeshi letu la anga linachukua majukumu makubwa katika kuondoa vitisho kwa usalama wa nchi yetu, haswa katika mapambano dhidi ya ugaidi," alisema.

Akizungumzia Operesheni ya "Claw-Lock" inayoendelea, iliyoanzishwa mwaka wa 2022 kulenga maficho ya magaidi wa PKK kaskazini mwa Iraq, Erdogan alisema kwamba watahakikisha kwamba watu wanaotaka kujitenga sio tena chanzo cha tishio kwa "taifa letu na ndugu zetu wa Iraqi."

Erdogan alisema baadhi ya washirika, badala ya kuunga mkono Uturuki, "hawakusita kuunga mkono kwa uwazi upanuzi wa PKK wa Syria na kuwakaribisha kawa zulia jekundu viongozi wa kundi la kigaidi linalotaka kujitenga ."

"Tunategemea nguvu na uwezo wetu peke yake," aliongeza.

Erdogan pia alipongeza Jeshi la Uturuki kwa kukabiliana na changamoto, ikiwa ni pamoja na mapinduzi yaliyoshindwa 2016 yaliyoratibiwa na Shirika la Kigaidi la Fetullah (FETO).

"Hatukung'oa tu genge la uhaini la FETO ambalo lilikua kama uvimbe mbaya kwa takriban miaka 40, lakini pia tuliimarisha jeshi letu katika kila nyanja," alisema.

Rais alisema kuwa Uturuki imeshikamana na "marafiki na ndugu zake popote inapohitajika."

Ankara imeunga mkono washirika wake huko Libya, Somalia na Azerbaijan, rais alisema, akisisitiza kwamba hakuna jeshi lolote duniani, isipokuwa Jeshi la Wanajeshi wa Uturuki, ambalo lingeweza kupata mafanikio hayo nje ya mipaka yake kwa "muda mfupi sana."

TRT World