"Ninaamini kuwa hatua za ziada zitaendelea kuchukuliwa ili kuimarisha haki za Waturuki wa Kitatari wa Crimea katika kipindi kijacho," anasema Erdogan. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza tena ahadi ya Ankara kuunga mkono mamlaka kamili ya eneo la Ukraine.

"Uungaji mkono wetu kwa mamlaka ya eneo na uhuru wa nchi ya Ukraine, mamlaka na uhuru hauteteleki," Erdogan alisema Jumatano katika ujumbe wa video uliotumwa kwa Mkutano wa Nne wa Viongozi wa Kongamano la Crimea.

"Kurejeshwa kwa eneo la Crimea chini ya udhibiti wa Ukraine ni sharti la sheria za kimataifa," Erdogan alitangaza.

Aliangazia msimamo wa Uturuki kuhusu Crimea, akisisitiza kuwa kurejeshwa kwa eneo hilo Ukraine kunawiana na viwango vya kisheria vya kimataifa.

Erdogan pia alionyesha imani katika hatua zinazochukuliwa kusaidia Waturuki wa Kitatari wa Crimea, akisema: "Ninaamini kuwa hatua za ziada zitaendelea kuchukuliwa ili kuimarisha haki za Waturuki wa Kitatari wa Crimea katika kipindi kijacho."

Erdogan aliwasilisha nia ya Ankara ya kumaliza mzozo na Urusi, akisema, "Matamanio yetu ya dhati ni kwamba vita vimalizike kwa amani ya haki na ya kudumu kwa misingi ya mamlaka kamili ya eneo, na uhuru wa nchi ya Ukraine."

Kufanya Crimea kuwa sehemu ya nchi nyingine

Vikosi vya Urusi viliikalia Rasi ya Crimea mnamo Februari 2014, na Rais wa Urusi Vladimir Putin aligawanya eneo hilo kuwa sehemu mbili za Shirikisho la Urusi mwezi uliofuata.

Tangu wakati huo, Watatari wa Crimea wameendelea na mapambano yao ya kupigania mamlaka kamili ya eneo la Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Watatar wa kabila la Crimea wamekabiliwa na mateso tangu Urusi ilipochukua rasi a hiyo mwaka 2014, hatua ambayo Uturuki imeikashifu.

Uturuki na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wanalitaja unyakuzi wa Urusi kama kinyume cha sheria.

TRT Afrika