Uturuki ni mzalishaji mkubwa wa ndege zisizo na rubani ulimwenguni, huku makampuni ya Uturuki yakiwa yamefikia asilimia 65 ya mauzo ya ndege vita za kijeshi duniani kuanzia mwaka 2018./Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa Uturuki haitoridhika mpaka iwe imeondoa vitisho vyote vya magaidi katika vyanzo vyao.

"Iwe ndani au nje ya mipaka yetu, hakuna wa kutuzuia kuondoa vitisho dhidi ya nchi yetu," alisema Erdogan katika risala yake aliyoitoa katika makao makuu ya Kiwanda cha Anga cha Uturuki (TAI) jijini Ankara siku ya Jumanne, ambacho wiki iliyopita kilishambuliwa na magaidi na kusababisha vifo vya watu watano.

Kulingana na Erdogan, matukio ya namna hiyo hayatovunja nia ya Uturuki ya kupambana na ugaidi.

Huku akiliita shambulio la kundi la kigaidi la PKK dhidi ya TAI kama "juhudi za mwisho za shirika linalotaka kujitenga," Erdogan alisisitiza kuwa ugaidi hauna nafasi katika siku zijazo za Uturuki.

Katika miaka yake 40 ya kufanya ugaidi dhidi ya Uturuki, kikundi cha PKK kinatajwa kama taasisi ya kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, ikihusika na vifo zaidi ya 40,000, vikiwemo vya wanawake, watoto na wachanga.

Akizungumzia sekta ya ulinzi ya Uturuki, Rais wa Uturuki alisema," Tumekuwa nchi inayojitegemea katika eneo hili, tukiwa na miradi ya ndani zaidi ya elfu moja yenye thamani ya dola bilioni 100."

"Leo hii, umuhimu wa mfumo wetu wa usalama wa anga umekubalika zaidi," ameongeza.

Amesema Uturuki ni mzalishaji mkubwa wa ndege zisizo na rubani ulimwenguni, huku makampuni ya Uturuki yakiwa yamefikia asilimia 65 ya mauzo ya ndege vita za kijeshi duniani kuanzia mwaka 2018.

"Kama wana uzio wa chuma, basi sisi tutakuwa na uzio wa bati," alisema, akiongeza kuwa Uturuki itaimarisha uwezo wake wa makombora ya mbali.

"Hatutosimama wala kupumzika mpaka tufikie azma yetu ya kuwa Uturuki huru iliyo kamilifu katika sekta ya ulinzi," Rais wa Uturuki alisisitiza.

"Tutafanya kazi kwa nguvu zaidi kupambana na wasaliti; tutazalisha zaidi kuwadhibiti wahuni hao; tutaendeleza zaidi kuwadhibiti mabeberu."

TRT Afrika