Maonyesho makubwa ya Uturuki ya anga na teknolojia, Teknofest, yanaanza Jumatano katika mji wa Adana uliopo kusini, yakiahidi siku tano za shamrashamra ya kusherehekea ubunifu na teknolojia katika Uwanja wa ndege wa Adana Sakirpasa.
Sherehe hiyo itaonyesha mambo kadhaa, ikiwemo maonyesho ya ndege za vita, ndege zisizo na rubani, na helikopta, pamoja na warsha, makongamano na mashindano.
Onyesho la mwaka huu, litaangazia mashindano ya teknolojia katika nyanja mbalimbali kama vile usafiri wa kisasa, uundaji wa roketi na roboti, ndege zisizo na rubani, na mifumo ya chini ya maji isiyoendeshwa na binadamu.
Kuonyesha moyo wa mashindano, shindano hilo litahodhi ufunguzi wa Ligi ya Teknofest, ambapo washindi kutoka mashindano ya teknolojia yanayohusisha timu 790,000 na zaidi ya washiriki milioni 1.65 watashindania zawadi ya fedha za Kituruki kiasi cha 500,000 (takriban $14,600).
Shindano hili litafanyika kwa zaidi ya siku tatu na lina lenga kuonyesha timu bora za teknolojia nchini.
Ikiratibiwa na Turkish Technology Team Foundation (T3 Foundation) kwa kushirikiana na Wizara ya Uturuki ya Viwanda na Teknolojia, Teknofest ina historia ndefu ya kufanyika katika miji kadhaa ya Uturuki.
Tukio hilo linafanyika nje ya Istanbul katika miaka yenye namba shufwa, na katika miji mikubwa katika miaka yenye namba witiri.
Mwaka jana, kuadhimisha karne ya Jamhuri ya Uturuki, sherehe hiyo ilifanyika katika maeneo matatu: Istanbul, mji mkuu Ankara, na mji wa Izmir.