Erdogan alikutana na Musk Katika jengo la Uturuki kando ya kikao cha 78 cha Mkutano mkuu wa UN, UNGA. / Picha: AFP

Mkurugenzi mtendaji wa Tesla Elon Musk ana "uwezekano mkubwa" wa kutembelea mji wa Izmir nchini Uturuki kushiriki maonyesho makubwa zaidi ya Teknolojia na anga maarufu TEKNOFEST, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema.

Rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan, na Elon Musk walikutana mjini New York na kujadili uwekezaji wa Tesla nchini Uturuki, na hatua za pamoja katika masomo ya 'space'.

"Nimemwalika Izmir TEKNOFEST. Ana uwezekano mkubwa wa kuja maonyesho hayo ya TEKNOFEST, " Erdogan alisema akizungumza na waandishi wa Habari jijini New York.

"Yeye (Elon Musk) naye alisema,' nimesikia mambo mazuri kuhusu Izmir, na nitajaribu kuhudhuria Izmir Teknofest."Wenzetu watawasiliana nao," Erdogan alisema.

Aidha, Erdogan emongeza kuwa alijadili na Musk kuhusu " uwekezaji wa Tesla nchini Uturuki na hatua za pamoja katika masomo ya anga.”

"Yeye (Elon Musk) alisema kwamba alifuata UAV ya Uturuki (gari la anga lisilo na rubani) na UCAV (gari la anga lisilo na silaha) na kuziona zenye mafanikio.

Anajua mafanikio ya nchi yetu katika sekta ya teknolojia haswa miaka ya hivi karibuni. Hii pia itakuwa ushawishi wa kuhamisha uwekezaji wake kwenda Uturuki, " aliongeza.

Rais wa Uturuki pia alimjulisha Musk kuhusu "mafanikio ya kiteknolojia ya Uturuki pamoja na maono ya 'Uturuki Dijitali' na Mkakati wa Kitaifa wa Akili Bandia", Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki ilisema katika taarifa.

AA