Makala ya kwanza ya TEKNOFEST, yalifanyika katika Uwanja wa ndege wa Istanbul 2018.
Tamasha hilo chini ya kauli mbiu, "Kwa sababu wewe ni Mustakbali" itakuwa ni ndio makala ya mwisho ya TEKNOFEST mwaka huu chini ya uratibu wa (T3) Wakfu wa Timu ya Teknolojia Uturuki na Wizara ya Viwanda na Teknolojia.
Tamasha hilo, ambalo ni la tatu mwaka huu, baada ya kufanyika Istanbul kati ya Aprili 27 na Mei 1, na baadae kufanyika Ankara kwenye maadhimisho ya Miaka 100 ya uwepo wa Jamhuri ya Uturuki, sasa litafanyika Izmir kati ya Septemba 27 na Oktoba 1, na kuwapokea wapenzi wa masuala ya teknolojia mjini Izmir.
Maonyesho mbalimbali yameratibiwa kufanyika yakiwemo ya teknolojia, mashindano ya ujasiriamali katika maonyesho ya anga, maonyesho ya sayansi na michezo na matamasha mbalimbali yatakayofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Çiğli, mjini Izmir.
Vitengo viwili vipya kushindaniwa
Kwa mara ya kwanza, vitengo viwili vipya vimejumuishwa na vitashuhudiwa katika makala ya TEKNOFEST Izmir, yakiwemo shindano maarufu ya 'Jaribu Utekeleze' na 'Makeathon.'
Ndani ya wigo la tamasha, timu 913 kutoka wanafuzi wa shule za msingi na wanafunzi elfu 2,592 wa shule za upili na kwenda mbele kutoka mikoa 81 na vitengo 132 tofauti vya Teknolojia ya Majaribio wamejiandikisha kushindana kwenye tamasha hilo.
Aidha katika mashindano ya kufuzu ambayo wanafunzi walifanya miradi wakiungwa mkono na washauri wao, jumla ya timu 327 na wanafunzi 1055 walijishindia tiketi ya kushiriki maonyesho.
Tangu makala ya 2018, TEKNOFEST imevutia washiriki mbalimbali wakiwemo Timu 4333 na vijana elfu 20 waliowasilisha maombi ya kushiriki mashindano ya teknolojia yaliyofanyika.
Aidha, mpaka sasa wageni zaidi nusu milioni wamehudhuria tamasha hili.
Zawadi yenye thamani ya zaidi ya lira milioni 2 pia zimetolewa pamoja na ufadhili wa kifedha unaozidi lira milioni 2 zitatolewa katika mashindano hayo.
Aidha watu elfu 943 walitembelea makala ya TEKNOFEST ya maadhimisho ya 100 ya Jamhuri ya Uturuki kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika uwanja wa ndege wa Ankara Etimesgut ikiwa ni mara yake ya kwanza katika mji mkuu huo.