Wageni katika tamasha la anga na teknolojia TEKNOFEST katika Uwanja wa Ndege wa Çiğli. / Picha: AA

Tamasha kuu la teknolojia na anga la Uturuki TEKNOFEST 2023 litafungua mkondo wake wa tatu na wa mwisho Jumatano katika jiji la Izmir Kusini-Magharibi mwa nchi.

Tukio hilo la siku tano litakamilika Oktoba 1 na limeandaliwa na Wakfu wa Timu ya Teknolojia ya Uturuki (T3) na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Uturuki.

Ni onyesho la kupendeza la maonyesho ya ndege, mashindano ya teknolojia, warsha za elimu, maonyesho ya programu na uzoefu maalum wa ndege.

Hafla ya mwaka huu inakuja wakati maalum ambapo Uturuki inaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.

Tukio hilo mwaka huu lilianza kwa mkondo wa kwanza wenye nguvu huko Istanbul mnamo Aprili, ambao ulirekodi wageni milioni mbili - na kuvunja rekodi zote za hapo awali.

Mkondo wa pili ulifanyika Ankara kati ya Agosti 30 na Septemba 3 kwenye Uwanja wa Ndege wa Etimesgut, ambao ulipokea wageni 943,000.

Izmir, inayefafanuliwa kuwa lulu ya Bahari ya Aegean, sasa imefurika watu kwa kishindo huku wakitumai kuweka rekodi yao wenyewe na kupeleka msisimko wa onyesho hili la kushangaza angani.

Hafla hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa Çiğli mjini Izmir na itakuwa na maonyesho kamili ya mashindano ya teknolojia na ujasiriamali, maonyesho ya anga, maonyesho ya vyombo vya usafiri vya ardhini na angani, shughuli za warsha ya elimu, maeneo ya uzoefu wa kuiga kati ya shughuli zingine.

TRT Afrika