Erdogan alitoa zawadi kwa Jeshi la Jamhuri ya Albania "idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani," kulingana na Rama, ambaye alionyesha shukrani zake. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani ukatili wa Israeli huko Gaza, na kuutaja kama "aibu ya pamoja kwa ubinadamu" katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Albania Edi Rama.

"Tunahitaji kufanya kila juhudi kama jumuiya ya kimataifa kuhakikisha usitishaji mapigano wa kudumu, kutoa misaada ya kibinadamu, na kutumia shinikizo linalohitajika kwa Israeli," Erdogan aliambia waandishi wa habari kufuatia mkutano wake na Rama katika mji mkuu wa Albania wa Tirana siku ya Alhamisi.

"Ninaamini kwa dhati kwamba Albania pia itafanya sehemu yake katika suala hili," aliongeza.

Erdogan na Rama pia waliongoza kikao cha pili cha Baraza la Ushirikiano wa Ngazi ya Juu na kusimamia utiaji saini mikataba minne ya ushirikiano katika nyanja za mawasiliano, elimu na kilimo, na kuthibitisha nia ya nchi hizo mbili kushirikiana.

Baadaye, Erdogan alizindua Msikiti Mkuu wa Tirana, unaojulikana pia kama Msikiti wa Namazgah.

Akihutubia umati uliokusanyika kwa sherehe hiyo, alisisitiza kuwa ni "wajibu wa dhamiri" kusimama dhidi ya "ugaidi wa serikali" wa Israeli.

Ndege zisizo na rubani za Uturuki nchini Albania

Wakati wa ziara yake, Erodgan alisisitiza kwamba Uturuki itatoa msaada unaohitajika kwa washirika wao wa kimkakati vikosi vya kijeshi vya Albania na vifaa vya kijeshi na mafunzo.

Rais alitoa zawadi kwa Jeshi la Jamhuri ya Albania "idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani," kulingana na Rama, ambaye alionyesha shukrani zake.

Erdogan yuko Tirana kama sehemu ya ziara ya Balkan, baada ya kukutana mapema na Rais wa Albania Bayram Begay.

Juhudi za pamoja kati ya Ankara na Tirana pia zinalenga kuongeza kiwango cha biashara baina ya nchi hizo mbili hadi dola bilioni 2 ndani ya awamu ya kwanza, kulingana na Erdogan, ambaye pia alijadili mapambano ya pamoja dhidi ya mashirika ya kigaidi kama vile FETO wakati wa mkutano wake na Rama.

Maelezo juu ya mikataba

Erdogan na Rama walitia saini azimio la pamoja la kuimarisha ushirikiano wa kimkakati unaoundwa na mabaraza ya ushirikiano wa ngazi ya juu ya serikali hizo mbili.

Wizara za kilimo na misitu za nchi hizo mbili pia zilitia saini azimio la nia ya kushirikiana katika nyanja ya bima ya kilimo inayofadhiliwa na serikali.

Mkataba wa maelewano (MoU) wa ushirikiano katika mahusiano ya umma na mawasiliano pia ulitiwa saini.

Kwa kuongezea, itifaki ilitiwa saini ili kuanzisha matawi ya kitaaluma na programu za Chuo Kikuu cha Ufundi cha Istanbul nchini Albania.

Ziara za kikanda za Erdogan zinatarajiwa kujumuisha mapitio ya kina ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Baada ya ziara yake nchini Albania, Erdogan atasafiri hadi mji mkuu wa Serbia Belgrade baadaye siku ya Alhamisi.

Msikiti Mkuu wa Tirana

Msikiti Mkuu wa Tirana, pia unajulikana kama Msikiti wa Namazgah, ni mmoja wa misikiti mikubwa zaidi katika Balkan.

Uturuki ni mshirika wa kimkakati wa Albania na mmoja wa wawekezaji wake wakubwa, akichangia katika miundombinu na sekta zingine.

Ujenzi wa msikiti huo mpya ulizinduliwa mwaka 2015 kwa takriban euro milioni 30 (dola milioni 34) kutoka kwa Urais wa Masuala ya Kidini (Diyanet).

Mbali na minara hiyo minne, msikiti wa Namazgah una kuba la kati la mita 30 na uwezo wa kutoshea watu 8,000.

Inakaa kwenye sehemu ya ardhi ya mita za mraba 10,000 karibu na bunge la Albania, na ghorofa ya kwanza inajumuisha kituo cha kitamaduni. Ina uwezo wa kutoshea watu 10,000 kuomba.

TRT World