Kulingana na Rais Erdogan, "vizuizi" ambavyo Uturuki ilikabiliana navyo vimeipa nchi hiyo hali ya kujitegemea kiulinzi. / Picha: AA  

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amegusia mageuzi ya nchi yake kwenye eneo la uwezo wa kiulinzi katika kipindi cha miaka 22, na kuyaita ya "kihistoria", licha ya vizuizi vya kimataifa.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa X siku ya Ijumaa, Erdogan alisisitizia safari ya Uturuki kutoka utegemezi wa vifaa vya kijeshi hadi hali ya kujitegemea na kuwa na uwezo wa kuzalisha yenyewe pamoja na kuuza.

“Tumejiandikia historia ya kipekee ndani ya miaka 22 iliyopita,” alisema Erdogan akigusia baadhi ya mafanikio kama vile “uzio wa chuma" mfumo wa ulinzi wa anga na teknolojia ya “Siper.”

Erdogan pia alisisitizia hatua iliyopigwa katika teknolojia ya satelaiti, akisema kuwa urushwaji wa IMECE, chombo cha kwanza cha uchunguzi wa anga za mbali, kunatoa fursa za kupata taswira mbalimbali za huko.

Aliangazia mradi wa TURKSAT 6A, ambao umeiweka Uturuki kati ya mataifa teule yenye uwezo wa kutengeneza satelaiti zao za mawasiliano.

Akizungumzia vizuizi vya kimataifa, Erdogan alisema kuwa vikwazi vimeipa nchi hiyo hali ya kujitegemea kiulinzi.

"Hatua ya kuelekea kujitegemea kiulinzi sio ya nchi yetu peke yake," alisema Erdogan "inadhihirisha mwanzo mpya kwa wale wanaonyanyaswa na ulimwengu mzima."

Tamko hilo linasisitiza juhudi zinazoendelea za Uturuki kujiimarisha kama mdau mkuu katika tasnia ya ulinzi ya kimataifa, huku vifaa vyake vya kijeshi sasa vinasafirishwa kwa nchi nyingi ulimwenguni.

Vifaa vya ulinzi kutoka Uturuki vyafikia nchi 178 ndani ya mwaka 2024

Kampuni mbalimbali katika sekta ya ulinzi ya Uturuki imesafirisha bidhaa kwa nchi 178 zilizovunja rekodi mwaka huu, alisema Rais wa nchi hiyo siku ya Ijumaa.

"Kwa mwaka 2024 pekee, kampuni zetu za ulinzi ziliweka rekodi nzuri kwa kusafirisha bidhaa kwa nchi 178 tofauti," Recep Tayyip Erdogan alisema katika Maonesho ya Kimataifa ya Ulinzi na Anga ya 2024 ya SAHA huko Istanbul.

Wakati wa hafla hiyo, ambayo pia hujulikana kama maonesho ya SAHA, mikataba yenye thamani ya dola bilioni 6.2 itatiwa saini, ikijumuisha dola bilioni 4.6 katika mikataba ya usafirishaji, Erdogan alisema, na kuongeza, "Hii ni kumbuku muhimu."

"Tutatumia ujuzi uliopatikana kutoka kwa miradi ya satelaiti ya TURKSAT 6A na IMECE katika kupanga na kutekeleza mradi wetu wa kwenda mwezini," Erdogan aliongeza.

TRT Afrika