Rais Recep Tayyip Erdogan alikuwa na mazungumzo ya simu na Rais wa Iran Ebrahim Raisi.
Katika mazungumzo hayo ya Jumapili, viongozi hao wamejadili uhusiano kati ya Uturuki na Iran, mashambulizi ya Israel dhidi ya maeneo ya Palestina, na hali ya kibinadamu katika eneo hilo.
Rais Erdogan alisema ni muhimu kuendelea kuongeza juhudi za kutekeleza uamuzi wa kusimamisha mapigano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huko Gaza haraka iwezekanavyo na kwamba Fatah na Hamas wanapaswa kufanya kazi kwa umoja katika mchakato huu.
Rais Erdogan pia alisema kuwa ni muhimu kufanya kazi pamoja ili kuzuia juhudi za Israel za kueneza mvutano katika eneo hilo.
Uchokozi wa Israel dhidi ya Palestina
Israel imefanya mashambulizi mabaya ya kijeshi huko Gaza tangu shambulio la Oktoba 7 kuvuka mpaka la Hamas ambalo liliua takriban watu 1,200.
Takriban Wapalestina 32,800 wameuawa na wengine 75,300 kujeruhiwa huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji.
Vita vya Israel vimewafanya asilimia 85 ya wakazi wa Gaza kukimbia nyumba zao huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, huku asilimia 60 ya miundombinu ikiwa katika hali mbaya, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
Mazungumzo na Rais wa Uzbek
Rais Erdogan pia alifanya mazungumzo ya simu na Rais wa Uzbekistan, Shavkat Mirziyoyev.
Masuala ya Kimataifa na Kikanda yalitawala mazungumzo baina ya viongozi hao.
Rais Erdogan alimshukuru Mirziyoyev kwa kumpongeza, kufuatia kufanikisha kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini Uturuki, uliendeshwa kwa ukomavu wa kidemokrasia.
Mahusiano ya nchi mbili yalijadiliwa na Caparov wa Kyrgyzstan
Rais wa Uturuki Erdogan alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais wa Kyrgyzstan, Sadyr Caparov.
Wakati wa mazungumzoi hayo, uhusiano wa nchi mbili kati ya Uturuki na Kyrgyzstan, pamoja na masuala ya kimataifa na kikanda, yalijadiliwa.
Rais Erdogan alitoa shukrani zake kwa Caparov kwa kutoa pongezi kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa ya Uturuki.