Leo ni siku muhimu katika historia ya mahusiano ya nchi za Uturuki na Somalia, wakati meli ya utafiti ya Uturuki, iitwayo Oruç Reis ikianza safari kuelekea nchini Somalia kwa shughuli za kitafiti.
Meli hiyo inatarajiwa kusafiri kupitia bahari ya Mediterani, mfereji wa Suez na kisha bahari Nyekundu kabla ya kufika pwani ya Somalia. Meli ya Oruç Reis, inatarajiwa kufika Somalia mwishoni mwa mwezi Oktoba, na itafanya tafiti za jiolojia kuhusu uwepo wa gesi asilia na mafuta katika eneo hilo.
Chombo hicho kitafanya tafiti mbalimbali katika eneo hilo, shughuli ambayo itachukua miezi 7. Meli ya Oruç Reis itakusanya taarifa muhimu kuhusu uwepo wa gesi asilia na mafuta na kisha taarifa hizo kuchambuliwa jijini Ankara, kabla ya kuanza kwa shughuli ya uchimbaji wa rasilimali hizo.
Meli hiyo, iliyotengenezwa nchini Uturuki, ina urefu wa mita 87, upana wa mita 23 na urefu wa mita 34.