Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amesisitiza katika mkutano wake na mwenzake kutoka Marekani Antony Blinken umuhimu wa kusitisha mauaji ya Gaza, haraka iwezekanavyo.
Wakati wa mkutano katika mji mkuu wa Saudi Riyadh siku ya Jumatatu, Fidan alisema shinikizo linapaswa kutolewa kwa Israel kwa ajili ya kukomesha mauaji hayo, usitishaji wa kudumu wa mapigano, na kuwasilisha misaada ya kibinadamu Gaza.
Fidan na Blinken pia walijadili hali ya hivi karibuni huko Gaza, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.
Hali ya sasa ya Ukraine na uhusiano wa pande mbili kati ya Ankara na Washington pia yalitawala mazungumzo ya wanadiplomasia hao .
Mkutano wa Kikundi cha Mawasiliano kwa Gaza
Fidan na Blinken walikutana pembezoni mwa mkutano wa Kikundi cha Mawasiliano cha Gaza, kinachofanyika kando ya Jukwaa la Kiuchumi la Dunia la siku mbili, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema kwenye ukurasa wake wa X.
Kundi la Mawasiliano la Gaza lilianzishwa katika mkutano wa kilele wa OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu huko Saudi Arabia mnamo Novemba ili kusimamisha mzozo wa Gaza na kusaidia kupatikana kwa amani ya kudumu.
Israel imefanya mashambulizi ya kikatili kwenye eneo la Palestina tangu shambulio la kuvuka mpaka la Hamas Oktoba 7 mwaka jana.
Takriban Wapalestina 34,500 wameuawa tangu wakati huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 77,600 kujeruhiwa huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba mkubwa wa mahitaji.