Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ahudhuria mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Astana, New York

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ahudhuria mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Astana, New York

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan ameshiriki kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jukwaa la Astana Jijini New York, Marekani
Mkutano wa Fidan na Mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov na Mwenzake wa Irani Hussein Emir Abdullahiyan. Picha: AA

Waziri wa mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amehudhuria mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jukwaa la Astana, New York.

Wizara ya Mambo ya Nje iliandika Kwenye mtandao wa X ya kuwa Fidan alihudhuria mkutano huo na ilichapisha picha yake akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Huseyin Emir Abdullahiyan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov.

Aidha, Fidan pia alimpokea mwenzake wa Saudi Faisal bin Farhan katika Jengo la Uturuki, au Kituo cha Turkevi, jijini New York.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Uturuki, ambaye yuko New York kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, awali alifanya majadiliano na wawakilishi na wenzake kutoka nchi tofauti.

AA