Mfumo wa sasa wa kimataifa, bila kuwepo dhana za mshikamano, haki na uaminifu, utashindwa hata kutimiza hata majukumu yake ya madogo, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.
Akihutubia Kongamano la Kidiplomasia la Antalya (ADF), ambalo limeanza katika mji wa Türkiye ulioko kwenye pwani ya Mediterania wa Antalya, rais wa Uturuki alisema Ijumaa kuwa mizozo ya Syria, Yemen, Libya na Ukraine inaonesha kushindwa kwa mfumo wa sasa wa kimataifa.
"Karne ya 21 inageuka kuwa zama ya migogoro, tofauti na ilivyotegemewa, na kupoteza maana ya utaratibu wa kimataifa unaozingatia kanuni na kuwa 'si zaidi ya kauli mbiu'," Erdogan alisema.
Anguko la utaratibu wa kidunia
Akizungumzia namna mgogoro wa Gaza kama ushahidi wa kuanguka kwa utaratibu wa sasa wa kidunia, Rais huyo wa Turkish anasema "Kinachotokea Gaza sio tu ni mgogoro, ni jaribio la mauaji ya kimbari-kwani hata vita vyenyewe vina sheria zake."
Wakati vita vya Palestina katika eneo la Gaza vinaingia siku yake ya 147, Rais wa Uturki ameonesha ni kwa namna gani watoto, wanawake na raia wasio na hatia wanavyouwawa kinyama Gaza.
Vilevile, alisisitiza namna mchakato huo unavyo tia doa imani ya watu kwenye haki na mfumo wa kidunia, akaongeza:
"Ninazungumzia usaliti na matendo yasiyo na staha wala heshima."
Akikosoa utaratibu wa sasa wa kimataifa na waungaji mkono wa Israel, alisema "Dola za Magharibi ambazo zinaiunga mkono Israel bila masharti tangu mwanzo zinashirik umwagaji damu kupitia sera zao za kinafiki."
Mashambulizi ya kikatili katika eneo la mzunguko wa Al Nabulsi
Akiangazia mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakisubiria msaada katika eneo la mzunguko wa Al Nabulsi katika eneo la Gaza lililozingirwa, Rais wa Uturuki Erdogan alisema, "Uturuki inafuata ukatili wa Israel kwa wasiwasi mkubwa."
Shambulio hilo la Alhamisi wakati wa utoaji wa misaada kaskazini mwa Gaza limeua Wapalestina 112.
Rais wa Uturuki aliongeza, "Jumuiya ya kimataifa inaweza tu kulipa deni lake kwa watu wa Palestina kupitia kuanzishwa kwa taifa la Palestina," akisisitiza matamshi ya Ankara juu ya ulazima wa kuundwa kwa taifa huru la Palestina lenye uadilifu wa ardhi, na mji mkuu Jerusalem Mashariki kwa msingi wa mipaka ya 1967.
Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya unagusia mambo kadhaa ya kidunia
Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya umeleta pamoja wajumbe kutoka nchi 147, na wastani wa washiriki 4,500, ikiwa ni pamoja na wakuu wa nchi 19, mawaziri 73, na wawakilishi 57 wa kimataifa..
Ikiwa na kauli mbiu ya "Kukuza Diplomasia Wakati wa Migogoro," kongamano hilo linaangazia masuala mbalimbali ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa hali ya hewa, uhamiaji, kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu, vita vya kibiashara, na akili mnemba.
Kongamano hilo linawaleta pamoja zaidi ya wanajopo zaidi ya 50, sanjari na maonesho mbalimbali.
Aina mbalimbali za washiriki ni pamoja na wanadiplomasia, wanasiasa, wanafunzi, wasomi, pamoja na wawakilishi kutoka asasi za kiraia na jumuiya za wafanyabiashara.
Kati ya maonesho kabambe ni "Karne ya Uturuki", yenye kuonesha maono ya Uturuki na mchango wake katika nyanja za sanaa, nishati, ulinzi na viwanda.
Jukwaa hilo pia linawasilisha "Maonesho ya Wachoraji Watoto wa Gaza."
Maonesho haya yameandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, yanatoa mtazamo wa kipekee kuhusu mgogoro wa kibinadamu huko Gaza kupitia macho ya watoto.