| Swahili
UTURUKI
1 DK KUSOMA
Ajali ya helikopta ya ambulansi yaua watu wanne  Uturuki
Ajali ya helikopta ya ambulensi huko Mugla, mkoa wa kusini magharibi wa Uturuki, na kuua marubani wawili, daktari na mfanyakazi wa afya.
Ajali ya helikopta ya ambulansi yaua watu wanne  Uturuki
Timu za zimamoto, afya na polisi pamoja na wafanyakazi kutoka Mamlaka ya Kudhibiti Maafa na Dharura ya Uturuki (AFAD) walitumwa kwenye eneo la tukio. / Picha: AA / Others
22 Desemba 2024

Helikopta ya ambulensi ilianguka katika hospitali katika mkoa wa Mugla kusini magharibi mwa Uturuki, na kuua watu wanne, kulingana na gavana wa jimbo hilo Idris Akbiyik.

Marubani wawili, daktari mmoja na mhudumu mmoja wa afya walipoteza maisha wakati helikopta hiyo ilipoanguka kwenye jengo la Hospitali ya Mafunzo na Utafiti katika wilaya ya Mentese ya Mugla.

Timu za zimamoto, afya na polisi pamoja na wafanyakazi kutoka Mamlaka ya Kudhibiti Maafa na Dharura ya Uturuki (AFAD) walitumwa kwenye eneo la tukio.

Akibainisha kuwa kuna ukungu mkubwa, Akbiyik alisema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa.

Akitoa salamu za rambirambi kwa waliofariki, Akbiyik alisema hakukuwa na uharibifu wowote ndani ya hospitali hiyo.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika