"Ninalaani vikali shambulio baya lililotekelezwa kwenye soko la Krismasi huko Magdeburg, Ujerumani, jana jioni," Erdogan alisema. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulizi katika soko la Krismasi katika mji wa Magdeburg nchini Ujerumani na kuua watu watano na kujeruhi wengine zaidi ya 200.

"Ninalaani vikali shambulio baya lililotekelezwa kwenye soko la Krismasi huko Magdeburg, Ujerumani, jana jioni," Erdogan alisema kwenye X siku ya Jumamosi.

Alituma rambirambi zake kwa familia za waliopoteza maisha katika shambulio hilo, na kwa "watu wenye urafiki na serikali ya Ujerumani."

Pia amewatakia afueni ya haraka majeruhi hao. Idadi ya watu waliofariki kutokana na shambulio la magari katika soko la Krismasi katika mji wa Magdeburg nchini Ujerumani iliongezeka hadi watu watano, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Jumamosi.

Shambulio hilo lilitokea Ijumaa katika soko maarufu la Krismasi katikati mwa jiji la Magdeburg.

Video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha gari jeusi likiingia kwa kasi kwenye umati, na kusababisha watu kukimbia kwa hofu na kusababisha fujo kwenye mkusanyiko wa sherehe.

Mhusika alikamatwa baada ya shambulio hilo. Polisi walidumisha ulinzi mkali katika soko la Krismasi na kuzingira eneo hilo ili kulinda eneo la uhalifu.

Viongozi wa eneo hilo wamewataka wakazi kuepuka eneo hilo wakati uchunguzi ukiendelea

TRT World