Majeruhi wa Kipalestina wafikishwa kwenye hospitali za Kuwait kwa matibabu kufuatia mashambulizi ya Israel katika mji wa Rafah. / Picha : AA  

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema wito wa kuwepo kwa amani huko Gaza, ambako Israel imeua zaidi ya watu 28,000, "bado haujazaa matunda kutokana na mtazamo hasi unaoonyeshwa na Marekani."

"Pamoja na Marekani kudai kuwatuma baadhi ya viongozi wa ngazi za juu katika kanda hiyo ili kutatua suala hilo, bado matokeo hayajapatikana.

"Ubinadamu lazima usikie kilio hiki haraka iwezekanavyo. Wajibu na uwajibikaji wa kukaa kimya katika kukabiliana na mauaji haya ya kimbari ni kubwa," alisema.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

"Hata hivyo, pamoja na hali hiyo tunaendelea kutafuta amani japo hatuoni njia mbadala," Erdogan alisema.

"Historia itawahukumu wale walioruhusu haya ya makusudi. Wale walioshiriki kwenye mauaji haya tayari wana hatia mbele ya historia," aliongeza.

TRT Afrika