Awamu mpya ya kudhibiti machafuko ya Syria iko katika hatua nzuri, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemwambia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, Rais Erdogan alikuwa na mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Alhamisi wakati wa mkutano wa Baraza la Taifa la Usalama kujadili masuala nyeti ya kikanda huku msisitizo ukiwa kwa Syria.
Wakati wa mazungumzo hayo, Erdogan alisistiza kuwa mgogoro wa Syria ulikuwa umeingia awamu nyingine kwa utulivu.
Kutengeneza njia ya maendeleo ya michakato ya kisiasa
Pia alisisitiza kuwa uzuiaji wa mapigano na ulinzi wa raia wa Syria ni moja ya vipaumbele vikuu vya Uturuki.
Erdogan alisisitizia msimamo wa serikali yake kuwa ni muhimu kwa utawala wa Syria kufanya kazi kwa ukaribu na watu wake kufikia suluhu ya kisiasa.
Rais wa Uturuki pia aliweka msisitizo wa katika juhudi za Uturuki za kupunguza vurugu na kuwalinda raia kwa ajili ya maendeleo ya michakato ya kisiasa, akisisitizia utayari wa nchi yake kufikia malengo hayo.
Juhudi za Ankara kwa suluhu ya kidiplomasia
Uturuki imekuwa mstari wa mbele katika kutatua mgogoro wa Syria, ikiwemo kuwa mwenyeji wa mamilioni ya wakimbizi kutoka Syria.
Nchi hiyo pia imefanya jitihada za kidiplomasia ikiwemo mazungumzo ya amani ya Astana, yanayolenga kuchochea mijadala kati ya pande zinazohasimiana.
Ukiwa umedumu toka mwaka 2011, mgogoro wa Syria umeisambaratisha kanda, ukisababisha mateso kwa binadamu.
Huku mgogoro huo ukiendelea, Uturuki inaendelea kuwa mtetezi wa maridhiano ya amani.
Mazungumzo kati ya Rais Erdogan na Guterres yanathibitisha msimamo wa Uturuki wa kutafuta suluhisho endelevu na utayari wake wa ushirikiano wa kimataifa wa kutatua moja ya migogoro mikubwa katika historia.