Erdogan atoa wito wa kuchukuliwa hatua kali za kimataifa dhidi ya Israeli kabla ya mkutano wa UN

Erdogan atoa wito wa kuchukuliwa hatua kali za kimataifa dhidi ya Israeli kabla ya mkutano wa UN

Ni muhimu kwamba jumuiya ya kimataifa, hasa UN, ipaze sauti yake kwa nguvu zaidi, anasema Recep Tayyip Erdogan.
Erdogan alisisitiza haja ya mfumo wa utawala wa kimataifa ambao unawakilisha kwa usawa mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kali zaidi, hususan Umoja wa Mataifa dhidi ya sera za Israeli za kuikalia kwa mabavu Palestina.

Katika ujumbe wa video kwa Wito wa Ulimwengu kuhusu Mkutano wa Kilele wa Siku za Usoni, tukio lililofanyika kupitia mtandaoni siku ya Alhamisi, Erdogan aliangazia Mkutano ujao wa Kilele wa Siko za Usoni kama fursa muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kimataifa na kufanyia kazi mfumo wa amani, usalama na haki wa kimataifa.

Ameutaja mkutano huo kuwa ni fursa adimu ya kushughulikia migogoro inayoendelea duniani, dhuluma, njaa na umaskini.

"Tunakabiliwa na hali ambapo zaidi ya watu 41,000 wamepoteza maisha, wakiwemo watoto 17,000, zaidi ya watu 100,000 wamejeruhiwa, na karibu Gaza yote imeharibiwa," Erdogan alisema.

"Katika kukabiliana na sera za uvamizi wa Israeli, ni muhimu kwamba jumuiya ya kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, kupaza sauti yake kwa nguvu zaidi. Katika ulimwengu ambao watoto wanakufa kutokana na mabomu, ninasema waziwazi kwamba hakuna hata mmoja wetu anayeweza kujisikia salama.

Kama Uturuki, tutaendelea kusimama dhidi ya ukandamizaji na pamoja na wanaokandamizwa, na hatutarudi nyuma kutoka kwa msimamo huu wa kibinadamu," aliongeza.

Haja ya mfumo mpya wa utawala wa kimataifa

Alitoa wito kwa washiriki wa mkutano huo kutumia kikamilifu fursa iliyotolewa na Guterres na kusisitiza haja ya amani ili kujenga mustakabali salama na wenye mafanikio.

Erdogan aliashiria athari kali za kijiografia na changamoto kama vile ugaidi, chuki dhidi ya wageni, na mabadiliko ya hali ya hewa, huku hali ya Gaza ikiwa mfano wa kutisha.

Rais pia alisisitiza haja ya mfumo wa utawala wa kimataifa ambao unawakilisha kwa haki mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea.

Alitetea mabadiliko ya mfumo unaozingatia mabadiliko ya kijani kibichi, uwezo wa kustahimili mabadiliko ya tabianchi, na maendeleo endelevu, kuhakikisha kuwa hakuna anayeachwa nyuma.

"Lazima tulinde demokrasia yetu dhidi ya aina zote za matamshi ya chuki, ubaguzi wa rangi, na watu wa mrengo wa kulia wenye na misimamo mikali ambayo inatia sumu jamii zetu," Erdogan alisema, na kuongeza kuwa ili kufikia malengo haya yote kuna haja ya kuunda upya mfumo wa kimataifa unaozingatia haki.

TRT World