Akizungumza katika shughuli ya “Mwaka wa Familia” jijini Ankara, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisisitizia umuhimu wa kuwalinda vijana wadogo dhidi ya itikadi zenye kutishia uhai wa familia.
Rais Erdogan alisema siku ya Jumatatu kuwa sera mbalimbali ikiwemo ile ya LGBT “zinatishia familia kama nguzo na taasisi imara."
"Maudhui haya ambayo yanaletwa kwa makusudi kabisa yana lengo la kuyumbisha na kudhoofisha familia zetu," alisema Rais Erdogan.
Pia alisisitiza kuwa Uturuki ni kati ya nchi ambazo zimepigia kelele suala hilo katika kila jukwaa ikiwemo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
"Lengo la sera hizi ni kudhoofisha familia."
"Tutaendelea kuweka wazi msimamo wetu hata katika siku zijazo," aliongeza. "Bila kujali watu watasemaj, msimamo wa Uturuki uko bayana, hatutowahi kurudi nyuma."