Waturuki watapiga kura katika raundi ya pili ya uchaguzi wa urais ambao rais alieko madarakani Recep Tayyip Erdogan huenda akampiku mpinzani wake mkuu Kemal Kilicdaroglu baada ya kukosekana mgombea aliyeweza kufikia kiwango cha asilimia 50 katika duru ya kwanza iliyo fanyika Mei 14.
Upigaji kura wa Jumapili utaanza saa mbili asubuhi [0500GMT] na kumalizika saa 11 jioni [1400GMT]. Kufikia Jumapili jioni kunapaswa kuwa na dalili ya wazi ya mshindi.
Zaidi ya watu milioni 60 wamejiandikisha kupiga kura, wakiwemo wapiga kura milioni 4.9 wapya. Jumla ya masanduku 191,885 ya kupigia kura yameundwa kwa ajili ya wapiga kura nchini.
Kulingana na Baraza Kuu la Uchaguzi la Uturuki, zaidi ya watu milioni 1.89 - 1,895,430 - tayari wamepiga kura zao katika vituo vya kigeni na lango la forodha la Uturuki kuanzia saa nne asubuhi [0700GMT] siku ya Alhamisi.
Upigaji kura katika balozi za kidiplomasia ulikamilika siku ya Jumatano, huku ukunuiwa kuwa utaendelea katika vituo vya forodha hadi saa kumi na moja jioni [1400GMT] siku ya Jumapili.
Katika uchaguzi wa Mei 14, jumla ya raia 1,839,470 wa Uturuki walioko nje ya nchi walipiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge.
Wale ambao hawataweza kupiga kura ndani ya muda uliowekwa maalum katika nchi wanamoishi wataweza kupiga kura kwenye lango la forodha hadi saa kumi na moja jioni kwa saa za kokote waliko siku ya Jumapili.
'Ushindi mkubwa wa Uturuki'
Siku ya Jumamosi, Erdogan alitoa wito kwa watu kujitokeza kupiga kura, akisema "tuanze Karne ya Uturuki na kura zetu."
"Kesho, twende kwenye uchaguzi pamoja kwa Ushindi Mkuu wa Uturuki. Wacha tuakisi nia ambayo ilidhihirishwa katika Bunge mnamo Mei 14 kwa Urais kwa nguvu zaidi wakati huu," Erdogan alisema kwenye Twitter.
Mamilioni ya wapiga kura walipiga kura Mei 14 kumchagua rais wa nchi hiyo na wabunge wake katika nafasi za viti 600.
Muungano wa watu wa Erdogan ulipata kura nyingi bungeni, huku kinyang'anyiro cha urais kikielekea raundi ya pili kwani hakuna mgombea aliyepata wingi wa kura au zaidi ya asilimia 50 ya kura inayo kubalika kikatiba ili kuwa mshindi.
Erdogan, 69, aliyaumbua maoni za nchi za Magharibi na akaibuka mbele kwa karibu pointi tano dhidi ya mpinzani wake Kemal Kilicdaroglu katika raundi ya kwanza.
Erdogan aliongoza kwa asilimia 49.52, huku Kilicdaroglu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Republican People's Party [CHP] na mgombea mwenza wa Muungano wa vyama sita vya upinzani Nation Alliance, akipata asilimia 44.9 ya kura.
'Natumai tutatembea pamoja'
Kambi ya Kilicdaroglu inajitahidi kurejesha kasi baada ya kupatwa na mshtuko katika raundi ya kwanza. Uchaguzi huo utaamua ni nani ataiongoza Uturuki, nchi ambayo ni mwanachama wa NATO na yenye wananchi milioni 85.
Uturuki pia ni nchi ambayo imechangia katika kusaidia wakimbizi na ina wakimbizi wengi duniani, ikiwa na wakimbizi milioni 5, kati yao milioni 3.3 wakiwa Wasyria, kulingana na takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mgombea wa nafasi ya tatu wa urais Sinan Ogan alisema anamuunga mkono Erdogan kwa kuzingatia kanuni ya "mapambano yasiyokoma dhidi ya ugaidi",akimaanisha kundi la kigaidi la PKK na matawi yake YPG, na FETO ambayo yalikuwa nyuma ya jaribio la mapinduzi lililoshindwa mwaka 2016.
Alipata asilimia 5.17 ya kura katika mkondo wa kwanza.