Jumla ya wataalam 60 wa ndani na nje ya nchi kutoka sekta ya umma, binafsi, vyombo vya habari, wasomi, taasisi za utafiti na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka takriban nchi 30 watashiriki. / Picha: AA

Mkutano wa Kimataifa wa kimkakati wa mawasiliano 2023 (Mkutano wa Stratcom), ulioandaliwa na kurugenzi ya mawasiliano ya Uturuki, utaanza rasmi katika jiji kuu la Uturuki la Istanbul.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atawahutubia washiriki na wajumbe kupitia ujumbe wa video katika mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu, mapambano ya kimataifa dhidi ya vitisho vya mseto: Utulivu, Usalama, Mshikamano.

Mkutano huo utaanza Alhamisi kwa hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na Mkurugenzi wa mawasiliano Fahrettin Altun.

Mkuu wa Mawasiliano ya Kimataifa wa Umoja wa Mataifa Melissa Fleming pia atatoa ujumbe wa video.

Washiriki wengine ni pamoja na Walid Ammar Ellafi, Waziri wa serikali ya Libya ya Mkataba wa Kitaifa, Zaid Makary, Waziri wa Habari wa Lebanon, Balozi Akif Cagatay Kilic, mshauri mkuu wa sera za kigeni kwa rais wa Uturuki, na Nancy Snow, Profesa mstaafu Katika Chuo Kikuu cha Jimbo la California.

Jumla ya wataalam 60 wa ndani na nje ya nchi kutoka sekta ya umma, binafsi, vyombo vya habari, wasomi, taasisi za utafiti na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka takriban nchi 30 watashiriki.

Takriban washiriki 3,000 wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa katika hafla hiyo.

Masuala mbalimbali yakiwemo kupambana na vitisho vya mseto kwa mawasiliano ya umma ya kidijitali, teknolojia mpya kwa akili bandia, migogoro ya kibinadamu kwa kujenga ujasiri wa kimataifa itajadiliwa kwa undani.

Ushirikiano wa mapambano ya kimataifa dhidi ya habari bandia na jukumu la Ankara katika kupambana na habari potofu pia itakuwa mojawapo ya mada za majadiliano ya jopo.

TRT World