Rais wa Uturuki Erdogan pamoja na rais wa Poland Duda kabla ya kikao cha 78 Cha Baraza kuu la UN katika Jengo la Uturuki, New York. / Picha: AA

Rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, Rais wa Poland Andrzej Duda na mwenzake wa Algeria Abdelmadjid Tebboune katika Jenga la Uturuki, New York kando ya mkutano mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, UN.

"Kama kawaida, tutaendelea kuwa mojawapo ya nchi zinazotoa mchango mkubwa kwa misheni ya NATO," Erdogan aliandika Kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa X, lililokuwa likujulikana hapo awali kama Twitter, muda mfupi baada ya mkutano na Stoltenberg,

Kwa upande wake, Stoltenberg alisema walijadili "kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi" na kumshukuru Rais Erdogan kwa juhudi za Uturuki ya kufufua mpango wa Nafaka wa Bahari nyeusi.

"Ilivyozungumzwa katika (mkutano wa NATO mnamo Julai huko) Vilnius, (Lithuania), bunge la Uturuki litaangazia Uanachama wa Nato Wa Sweden haraka iwezekanavyo," Stoltenberg aliandika Kwenye X muda mfupi baada ya mkutano huo, uliofanyika kando ya kongamano kuu la 78 la Baraza la Umoja wa mataifa.

Kuwalaki viongozi wa Poland na Algeria Katika Jengo la Uturuki

Aidha, Rais Erdogan pia amemkaribisha Rais wa Poland Duda Katika Jumba la Uturuki na kujadili masuala ya kikanda na mataifa hayo ikiwemo uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

"Natumai kuwa mkutano wetu na rais Duda utakuwa wenye manufaa kwa nchi na mkoa wetu," Erdogan alisema.

Mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan, Waziri wa viwanda na Teknolojia Mehmet Fatih Kacir, Waziri wa Biashara Omer Bolat na mkuu wa Shirika la Ujasusi la Kitaifa, Ibrahim Kalin, ulidumu takriban dakika 50.

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria pia alitembelea Erdogan Katika Jumba la Uturuki.

"Wakati wa mkutano huo, viongozi hao wawili walitathmini uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, masuala kwenye ajenda ya Umoja wa Mataifa, UN, pamoja na maendeleo ya kikanda na kimataifa," taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya Uturuki ilisema.

Mvutano unaoendelea barani Afrika na suluhisho zinazotolewa na nchi hizo mbili pia zilijadiliwa kwenye mkutano huo, taarifa hiyo iliongeza.

AA