Erdogan alikosoa mikakati ya Magharibi huko Ukraine na Gaza katika mkutano wa Nato. / Picha: AA

Wakati Rais wa Marekani Joe Biden akitafuta uungwaji mkono wa kimataifa huko Ukraine, huku mashambulizi ya Urusi yakiendelea, na kukosolewa kwa uungaji mkono wake kwa Israel katika vita vinavyoendelea dhidi ya Gaza, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Katika majibu ya maandishi ya kipekee yaliyotolewa na Newsweek, Erdogan, huko Washington, DC, kwa mkutano wa kila mwaka wa NATO, alikosoa mikakati ya Magharibi huko Ukraine na Gaza.

Erdogan alisema kuwa mataifa yenye nguvu ya Magharibi yalikuwa yakichukua njia zinazoweza kuwa hatari kwa mizozo yote miwili, ambayo alionya inaweza kuenea na kuwa makabiliano makubwa zaidi ya kikanda.

"Suluhu ni amani ya kudumu inayopatikana kupitia mazungumzo"

Kuhusu Ukraine, suala kuu lilokuwa katika mkutano wa NATO, Erdogan alisisitiza msimamo wake dhidi ya kujiunga na vita dhidi ya Urusi, licha ya wito wa Biden wa kutaka kuwe na umoja wa NATO dhidi ya Urusi.

"Suluhu sio umwagaji damu zaidi na mateso, lakini amani ya kudumu inayopatikana kupitia mazungumzo," Erdogan aliiambia Newsweek.

Alikosoa mikakati ya washirika wa Magharibi, akisema, "Mtazamo wa baadhi ya washirika wetu wa Magharibi dhidi ya Urusi umechochea moto tu. Hii imesababisha madhara zaidi kuliko manufaa kwa Ukraine. Kinyume chake, sisi tumekuwa na mazungumzo na pande zote mbili zinazopigana, katika juhudi za kuwaleta karibu na amani."

TRT World