"Mfumo wa kimataifa ulioanzishwa kulinda maslahi ya kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kidiplomasia ya washindi wa Vita vya Pili vya Dunia umeanza kupitwa na wakati," Erdogan alisema. /Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani Bunge la Marekani kwa kupongeza hotuba ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, aliyoitaja kuwa "iliyojaa wazimu."

"Ulimwengu mzima ulitazama na kuona jinsi muuaji wa mauaji ya halaiki alivyoshangiliwa katika Bunge la Marekani," Erdogan alisisitiza katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Kukuza Programu ya Juu ya Teknolojia huko Istanbul siku ya Ijumaa.

Akivutia hisia juu ya vita vya Israeli dhidi ya Gaza huko Palestina, ambayo sasa iko katika siku yake ya 294, rais huyo alisema: "Fikiria kuhusu wale walioua karibu watoto 40,000, wanawake na wazee; Baraza la Wawakilishi la linawapongeza."

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akihutubia Bunge la Marekani. /Picha: TRT World

Tel Aviv imewauwa takriban Wapalestina 39,175 - wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi wengine 90,403, huku zaidi ya watu 10,000 wakikadiriwa kuzikwa chini ya vifusi, tangu kuanza mashambulio yake makali dhidi ya eneo lililozingirwa mnamo Oktoba .

" Kama vile kusema, wale wanaofundisha ulimwengu mzima kuhusu demokrasia na haki za binadamu hawana wasiwasi juu ya kumheshimu Hitler wa wakati wetu," Erdogan alisisitiza, akipinga uungaji mkono wa Magharibi kwa mauaji ya Israeli dhidi ya Wapalestina.

Mfumo wa kimataifa 'uliopitwa na wakati'

Rais Erdogan wa Uturuki alizidi kukosoa mfumo wa kimataifa, akisema: "Tunakabiliwa na hali ya kuacha kutumia akili, unamualika mchinjaji ambaye ana damu ya watu elfu 150 wa Gaza mikononi mwake na, bila kutosheka na hilo, unapongeza hotuba yake iliyojaa wazimu."

Pia alisisitiza kuwa "mfumo wa kimataifa ulioanzishwa kulinda maslahi ya kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kidiplomasia ya washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia umeanza kupitwa na wakati."

Ikipuuza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano, Israeli imekabiliwa na shutuma za kimataifa kutokana na kuendelea na mashambulizi ya kikatili dhidi ya Gaza tangu shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na wapiganaji wa Palestina, Hamas.

Israeli inatuhumiwa kwa "mauaji ya halaiki" katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ambayo katika uamuzi wake wa hivi punde imeiamuru Tel Aviv kusitisha mara moja mashambulizi yake ya kijeshi huko Rafah kusini mwa Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni moja walikimbilia kutokana na vita vya Gaza. Rafah ilivamiwa Mei 6 na Jeshi la Israeli.

TRT World