Pazia la michuano ya Paris Olimpiki 2024, linafungwa leo nchini Ufaransa huku timu ya wanamichezo kutoka Tanzania ikirudi nyumbani bila medali yoyote.
Hata hivyo, kulingana na matokeo yaliyotolewa, Shauri alishika nafasi ya 40 40 kati ya Wanariadha zaidi ya 90 walioshiriki kwa upande wa wanawake, kwa kutumia muda wa saa mbili na dakika thelathini na moja na sekunde hamsini na nane (2:31:58) katika mashindano ya Olimpiki huko Paris, Ufaransa, wakati Sakilu alishindwa kumaliza mbio hizo.
Kwa mara nyingine tena, Tanzania imeshindwa kuwika kwenye mashindano hayo makubwa ulimwenguni.
Ikumbukwe kuwa wanariadha wa zamani Filbert Bayi na mwenzake Suleiman Nyambui, ndio waliofanikiwa kuiletea Tanzania medali kwenye mashindano hayo, wakifanya hivyo kwenye michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Moscow, Urusi mwaka 1980.
Katika mashindano ya Paris Olimpiki 2024, bendera ya Tanzania ilipeperushwa na wanamichezo 8, akiwemo waogeleaji Collins Saliboko na Sophia Latiff, mwanamasumbwi Yusuph Changalawe na mcheza judo Andrew Mlugu