Matumaini ya Tanzania kuvuna medali kwenye Michezo ya Olimpiki ya 2024 Paris sasa yapo kwa timu ya wanariadha 4 wanaoongozwa na Alphonce Felix Simbu ambaye atashiriki mbio za kilometa 42 kwa upande wa wanaume siku ya Agosti 11, 2024.
Mara ya mwisho kwa Tanzania kushinda medali za Olimpiki ilikuwa mwaka 1980, kupitia kwa Filbert Bayi na Suleiman Nyambui kwenye michezo ya Olimpiki nchini Urusi.
Tayari, wanariadha hao wanne ambao ni Simbu mwenyewe, Gabriel Geay, Magdalena Shauri na Jackline Sakilu wamewasili mjini Paris, tayari kabisa kwa mbio hizo.
Wakati Simbu na Geay watashiriki mbio za kilometa 42 kwa upande wa wanaume siku ya Agosti 10, 2024, Sakilu na Shauri wamepangwa kukimbia Agosti 11 kwa umbali wa kilometa 42, katika siku ambayo itahitimisha michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.
Licha ya kupeleka timu ya wanariadha katika makala za mashindano hayo makubwa ulimwenguni, Tanzania imeshinda kufanya vizuri kwenye michezo ya Olimpiki.
Ikumbukwe kuwa wanariadha wa zamani Filbert Bayi na mwenzake Suleiman Nyambui, ndio waliofanikiwa kuiletea Tanzania medali kwenye mashindano hayo, wakifanya hivyo kwenye michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Moscow, Urusi mwaka 1980.
Katika makala ya michezo ya Olimpiki ya jijini Moscow iliyofanyika mwaka 1980, Bayi alimaliza mbio hizo za mita 3000 na kutunukiwa medali ya fedha.
Kwa upande wake, Nyambui pia alishinda medali ya fedha kwenye mashindano hayo katika mita 5000.