Rais wa Nigeria Bola Tinubu amewakabadhi wachezaji na benchi la ufundi la 'Super Eagles' zawadi kabambe, ikiwemo nyumba na ardhi, baada ya timu hiyo kuhsika nafasi ya pili kwenye michuano ya AFCON 2023.
Akiilaki timu hiyo katika Ikulu ya Abuja, Tinubu amesema amejisikia fahari na timu hiyo, japo ilipoteza mchezo wake wa fainali dhidi ya wenyeji Ivory Coast.
Pamoja na kupoteza mchezo huo, kiongozi huyo hakuficha furaha na fahari yake, kutokana na kile alichokiita 'ustahimilivu' wa wachezaji wa Nigeria.
Kila mchezaji katika kikosi cha taifa alipokea Heshima ya Kitaifa ya (MON), heshima ya juu ya nchi, pamoja na majumba na ardhi katika eneo karibu na mji mkuu.
"Tuachane na tukio hili la kupita, lisituvunje moyo bali litulete pamoja ili tufanye kazi kwa bidii zaidi", akasema.
"Kwa wale vijana wa Nigeria wanaopendwa wanaonyesha zawadi zao katika jamii, wakichora mistari kwenye mchanga wanapocheza mpira wa miguu katika mstatili wao mnyenyekevu wa kucheza, unaweza kuwa mashujaa wetu kesho, usikate tamaa katika harakati zako.
"Utawala wangu uko hapa kutimiza ndoto," alisema.
Nahodha Msaidizi wa timu hiyo, Troost Ekong, ambaye pia ni mchezaji bora wa AFCON 2023, alimshukuru Rais Tinubu kwa heshima hiyo, akisema kuwa shauku yake ilikuwa kumkabidhi kiongozi huyo Kombe.