Morocco ilifika nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar. Picha: CAF

Ni miaka 47 tangu Morocco kushinda Afcon ingawa timu hiyo ilifanya vyema na hata kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana 2022, na kwa sasa ni moja wapo ya timu zinzatabiriwa kushinda taji hilo huko Ivory Coast.

Tangu kushinda kombe hilo mwaka 1976, Morocco imefika fainali mara moja tu, mnamo 2004 walipopoteza dhidi ya wenyeji Tunisia.

Kwenye makala ya mwisho yaliyofanyika nchini Cameroon mwaka 2022, walipoteza dhidi ya Misri katika robo fainali.

Regragui amehifadhi sehemu kubwa ya wachezaji wake walioshiriki Kombe la Dunia, na hata kuzaba Ubelgiji, Uhispania na Ureno kabla ya kutemwa kwa kufungwa 2-0 na Ufaransa katika nusu fainali.

Miongoni mwa waliodumishwa ni pamoja na Mlinzi wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi, Youssef En-nesyri wa Sevilla na Kiungo wa Manchester United Sofyan Amrabat.

Regragui amewatunuku Ismael Saibari wa PSV Na beki wa Real Betis Chadi Riad, ambaye alishinda AFCON kwa wachezaji chini ya miaka 23 mwaka huu wakiwemo baadahi ya vipaji vya vijana ili kufanikisha mchango wa wachezaji wa sasa na wa siku zijazo", alisema kocha huyo.

Simba hao wa Atlas watakabiliana na DR Congo, Tanzania na Zambia katika hatua za makundi kwenye mashindano hayo yatakayoanza Januari 13.

TRT Afrika