Victor Osimhen, Mwanasoka bora Afrika 2023 anaitumikia Nigeria kwenye michuoano ya AFCON/Picha:AFP

Victor Osimhen amekuwa msukuma kabumbu wa kwanza kutoka kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka 2023, baada ya Nwankwo Kanu mwaka 1999.

Osimhen, ambaye kilinda uso baada ya jeraha alilolipata Novemba 2021 akiwa mchezoni, alimaliza katika nafasi ya nane katika tuzo za Ballon D'or 2023, na kuwa Mnigeria wa kwanza kuwemo katika orodha ya wanasoka hao tajwa duniani.

Mbali na utambulisho huo mkubwa, Osimhen mwenye miaka 25, alichaguliwa kama mchezaji bora wa chini ya miaka 17 kwenye michuano ya CAF 2015.

Osimhen alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa Kiafrika katika Ligi ya Ufaransa, maarufu tuzo ya 'Marc-Vivien Foe'.

Kuteuliwa kwake kama mchezaji bora wa Serie A 2023 umemfanya kuwa mwafrika wa kwanza kutwaa tuzo hiyo na kuongoza kwa magoli katika ligi hiyo, na hivyo kuisaidia Napoli kushinda taji hilo toka msimu wa 1989–90.

Osimhen alishinda medali katika katika michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, ambapo pia aliibuka kuwa mfungaji bora kwa kuzifumania nyavu mara nyingi zaidi.

Osimhen ndiye Mnaigeria wa tatu kushinda taji la 'Scudetto' nchini Italia, baada ya Obafemi Martins na Victor Nsofor.

Anashikilia rekodi ya kufunga goli la haraka zaidi na kasi ya ajabu, katika historia ya Jupiler Pro League ya Ubelgiji.

Osimhen ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi zake tatu za kwanza katika ligi kuu ya soka Ufaransa, Ligue 1 wakati akiichezea Lille.

TRT Afrika