Klabu ya Liverpool imetoa tangazo hilo rasmi na kumshukuru Firmino kwa kuitumikia “The Reds” kwenye mechi 362 na kuiwezesha kutwaa mataji mbalimbali kipindi alichokuwa kwenye timu hiyo akifunga magoli 111 goals, na kutoa pasi za kufunga magoli 72.
Pindi Firmino anapofunga safari kuihama Liverpool, timu ndiyo imemsajili kiungo matata wa Hungary Dominik Szoboszlai kutoka klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig. Szoboszlai ni mchezaji wa pili kusainiwa na the Reds baada ya Alexis Mac Allister kuwasili kutoka Brighton ya Uingereza.
Firmino atajiunga na beki wa zamani wa Chelsea Kalidou Koulibaly wa Senegal kuichezea Al Hilal, mabingwa mara 18 wa ligi kuu ya Saudia ya Saudi Pro League.
Haya yanajiri baada ya kocha mpya wa timu hiyo Jorge Jesus kuwasili na kutua kwenye kambi ya mazoezi ya timu hiyo inayoendelea nchini Austria.