Diaz alitoa wito wenye hisia wa kuachiliwa kwa baba yake baada ya kufunga bao la kusawazisha kwa Liverpool katika sare yao ya 1-1 dhidi ya Luton, Jumapili. Picha: Getty

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliinua jezi kuonyesha ujumbe wake wa kuomba kuachiliwa kwa babake unaosomeka 'Uhuru Kwa Baba' na kisha akatoa taarifa akitaka "kuachiliwa kwake haraka" alipofunga bao la kusawazisha kwa Liverpool katika sare yao ya 1-1 dhidi ya Luton Jumapili.

Shirikisho la Soka nchini Colombia limethibitishwa kuachiliwa huru kwa Luis Manuel Díaz Jiménez, baba wa mchezaji wa Liverpool na timu ya taifa ya soka ya Colombia Luís Díaz.

"Shukrani kwa mamlaka kwa ajili ya kuachiliwa kwa Luís Manuel Díaz Shirikisho la soka la Colombia linashukuru Serikali ya Kitaifa, Jeshi na Vikosi vya Polisi vya Kitaifa, pamoja na taasisi zote na maafisa ambao waliwezesha kuachiliwa kwa Luís Manuel Díaz, baba wa mchezaji Wetu Luís Díaz." Shirikisho lilisema.

Novemba 5, 2023 Luis Diaz wa Liverpool asherehekea kufunga bao lake la kwanza kupitia Reuters

Kulingana na taarifa rasmi kutoka shirikisho la soka nchini Colombia, Luís Manuel Díaz, amfanikiwa kupata uhuru wake baada ya juhudi zilizohusisha serikali ya Kitaifa, jeshi na vikosi vya polisi vya kitaifa nchini humo, pamoja na taasisi mbalimbali za Colombia.

Diaz alitekwa nyara kwa bunduki na kundi la Jeshi la ukombozi wa taifa (ELN) mnamo 28 Oktoba pamoja na mkewe, Cilenis Marulanda, ambaye baadaye aliachiliwa kwa juhudi za polisi ndani ya masaa machache.

Hatimaye baada ya shughuli za utafutaji za kijeshi, serikali ilisema katika taarifa kwamba ilifanya mazungumzo ya amani na ELN na sasa ilikuwa ikisherehekea kuachiliwa kwa Diaz.

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kwamba babake Diaz alikuwa katika hali nzuri ya afya, bila kuwa na dalili za unyanyasaji na atasafirishwa kwa helikopta hadi eneo la Valledupar.

TRT Afrika