Klabu ya Liverpool imewasafirisha wazazi wa nyota wa Colombia Luis Diaz hadi England kuadhimisha msimu wa likizo na Krismasi huko England.
Liverpool ilikodisha ndege ya kibinafsi ambayo iliwasili Uingereza Jumamosi ikiwa na wazazi wa Diaz na wanafamilia wengine kutumia msimu wa sherehe Merseyside huku wakiendelea kupona kutoka kwa machungu ya kutekwa nyara nchi Colombia.
Luis Manuel Diaz, baba yake Diaz, aliachiliwa huru juma lililopita baada ya kushikiliwa kwa siku 12 na genge la ELN.
Baba yake Diaz alitekwa nyara akiwa na mkewe Cilenis Marulanda tarehe 28 Oktoba.
Marulanda aliokolewa saa chache baadaye kufuatia operesheni kubwa kupitia ardhi na anga iliyoanzishwa kumsaka pamoja na mumewe.
Luis Diaz alijawa na furaha alipoungana tena na wazazi wake aliporudi kwao Colombia kwa mechi ya kimataifa.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool aliishia kufunga mabao yote mawili katika ushindi wenye furaha wa 2-1 dhidi ya Brazil katika kufuzu Kombe la Dunia.
Diaz atajiunga na familia yake iliyowasili nchini England baada ya kuiwakilisha Colombia katika mechi ya kufuzu kombe la dunia siku ya Jumanne ugenini nchini Paraguay.