Mama wa winga huyo wa Liverpool Luis Diaz anayeiwakilisha timu ya taifa ya Colombia aliokolewa kutoka kwa watekaji nyara hao siku ya jumamosi lakini msako unaendelea ili kumpata baba yake, Rais wa Colombia Gustavo Petro alisema jumamosi.
Petro alichapisha kwenye mtandao wa X, ambayo zamani ilijulikana kama twitter, kwamba mama ya Diaz aliokolewa huko Barrancas kaskazini mwa nchi.
"Tunaendelea kumtafuta baba," aliongeza Petro.
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Colombia ilisema walikuwa wakifanya juhudi nyingi katika kesi hiyo.
Mamlaka zinashughulikia kesi hiyo
"Tangu ofisi ya mwanasheria mkuu ilipojulishwa juu ya utekaji nyara wa wazazi wa mchezaji wa Colombia Luis Díaz, katika eneo la Barrancas, La Guajira, kikosi maalum cha waendesha mashtaka, polisi na wanajeshi wamekuwa wakifanya kazi kuwaokoa" eneo la watu hawa, kufafanua ukweli na kupata wale wanaohusika, " ofisi hiyo ilisema Kwenye X.
Ripoti za vyombo vya habari vya eneo hilo zilisema kuwa, wanaume wenye silaha kwenye pikipiki waliwachukua wazazi hao Luis Manuel Diaz na Cilenis Marulanda walipokuwa katika kituo cha huduma katika sehemu ya La Guajira.
Mkurugenzi wa polisi, Jenerali William Salamanca, alisema alipeleka maafisa wa ujasusi na idara nyingine za polisi katika eneo hilo ili kushughulikia kesi hiyo.
Polisi " tayari wanahusika, hivi sasa, kutekeleza ukaguzi, kuwachunguza watu kwenye pikipiki, magari ya huduma ya umma ya kibinafsi kwa ajili ya kuwaokoa watu wawili waliotekwa nyara, baba na mama wa mwanasoka Luis Díaz," Salamanca aliambia vyombo vya habari vya Colombia mapema jumamosi.
Gavana wa La Guajira, Diala Wilches, alilaani utekaji nyara huo na kuomba warudishwe.
"Kwa watekaji nyara, tunawataka wawarudishe mara moja, salama salmini," alisema.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 26 hajatoa kauli kuhusu suala hilo.
Diaz ameiwakilisha Colombia mara 43 na alijiunga na Liverpool mwaka jana kutoka Porto.