Mashabiki wa Valencia wakiimba "Mono" (tumbili) kuelekea Vinicius | Picha: AA

Real Madrid ilifungwa 1-0 na Valencia katika mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania La Liga ambapo mashabiki wa Valencia walimtupia matusi ya kibaguzi mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr.

Bao la Diego Lopez dakika ya 33 lilileta ushindi kwa wenyeji Mestalla.

Baada ya dakika ya 67, Vinicius Jr alipoifungia Real Madrid mashabiki walianza kumtupia kejeli Mbrazil huyo.

Mechi hiyo ilibidi isimamishwe kwa dakika tisa huku matusi yakiendelea.

Vinicius alionyeshwa kadi ya njano awali kwa kumgombeza Hugo Duro wakati wa mzozo.

Lakini baada ya ukaguzi wa mwamuzi msaidizi wa video (VAR), kadi hiyo ilibadilika na kuwa nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 97.

Real Madrid wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 71, huku Valencia wakiwa katika nafasi ya 13 wakiwa na pointi 40.

Bosi wa Real Madrid aikosoa La Liga

Carlo Ancelotti, kocha mkuu wa Real Madrid, alishambulia La Liga baada ya mchezaji wake Vinicius Junior kulengwa na kashfa za ubaguzi wa rangi kwenye Uwanja wa Mestalla huko Valencia.

"Hii haikubaliki. La Liga ya Uhispania ina tatizo (la ubaguzi wa rangi), na sio Vinicius. Vinicius ndiye mwathirika." Kocha mkuu wa Real Madrid Ancelotti alisema katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi.

"... Uwanja mzima ulikuwa ukipiga kelele 'nyani, tumbili, tumbili'. Hakuna mengi ya kusema. Nina huzuni sana... Huwezi kucheza soka hivyo," kocha huyo wa Italia aliongeza.

AA