Klabu sita zikiwemo Bayern Munich, Inter, Real Madrid, Real Sociedad, Leipzig na Manchester City zimejihakikishia nafasi kwenye timu 16 bora msimu huu katika Champions League.
Bayern Munich imeshinda mechi zake zote za kundi A na kusalia kileleni kufuatia ushindi wake wa 2-1 dhidi ya Galatasaray ya Uturuki.
Klabu ya Arsenal inahitaji pointi moja tu kutoka mchezo wao ujao dhidi ya Lens ya Ufaransa ili kuvuka hadi hatua ya timu 16 bora.
Milan wanahitaji kushinda angalau moja kati ya mechi zake mbili zilizosalia ili kuendelea hadi hatua ya timu 16 bora.
Klabu ya Manchester United huenda ikaliaga kombe hilo iwapo itafungwa na Galatasaray katika mechi yake itakayofuata ya ugenini kwenye kombe la vilabu bingwa.
Miamba wa Uhispania, Barcelona bado wanatafuta tiketi ya kutua raundi ya mtoano kwenye Ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza katika misimu mitatu baada ya kufungwa na mabingwa wa Ukraine Shakhtar Donetsk 1-0 mjini Hamburg Jumanne.
Kwenye kundi F, Dortmund ya Ujerumani inahitaji ushindi dhidi ya Ac Milan ili kuelekea 16 ya mwisho na ikiwa hivyo ndio matokeo, ushindi wa PSG dhidi ya Newcastle pia utaiwezesha kufuzu hatua ya mtoano ya 16 bora.
- Kundi A: Bayern, Man United, Copenhagen, Galatasaray
- Kundi B: Sevilla, Arsenal, PSV Eindhoven, Lens
- Kundi C: Napoli, Real Madrid, Braga, Union Berlin
- Kundi D: Benfica, Inter, Salzburg, Real Sociedad
- Kundi E: Feyenoord, Atlético de Madrid, Lazio, Celtic
- Kundi F: Paris, Dortmund, Milan, Newcastle
- Kundi G: Man City, Leipzig, Crvena zvezda, Young Boys
- Kundi H: Barcelona, Porto, Shakhtar Donetsk, Antwerp
Aidha, timu itakayomaliza nafasi ya tatu kutoka kila kundi, itatinga moja kwa moja hadi kombe la UEFA Europa League, hatua za mchujo.
Kombe hilo la klabu bingwa ulaya litaendelea kwa msisimko wa hatua ya mtoano kuanzia Februari, huku mshindi wa mwisho akitawazwa katika Uwanja wa kifahari wa Wembley mjini London Jumamosi 1 Juni 2024.