Pogba anakabiliwa na marufuku ya miaka 4 iwapo vipimo vya sampuli "B" vitatoa matokeo chanya ya testosterone. / Picha: Getty

Kiungo wa Juventus na Ufaransa Paul Pogba amesimamishwa soka kwa muda baada ya uchunguzi wa dawa za misuli kuonyesha viwango vya juu vya testosterone, (homoni inayoimarisha misuli na mifupa mwilini, ambayo inakatazwa na mamlaka husika),

Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya nchini Italia NADO imesema.

Baada ya kuwa na msimu mbaya kati ya majeraha na sakata mbalimbali, ndoto za nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 za kufufua uwezo wake zilizamishwa na madai ya kosa la kutumia dawa za misuli baada ya ushindi wa Juventus wa 3-0 huko Udinese Mnamo Agosti 20, licha ya kutoshiriki mchuano huo.

Jumatatu hii, bingwa wa kombe la dunia 2018 aliiambia Al Jazeera juu ya "hamu yake ya kucheza baada ya" kupitia wakati mgumu ambao ungeweza kumharibu". Badala yake alipata pigo jipya.

NAIDOO ilisema kuwa Pogba alikiuka sheria za kupambana na dawa za kulevya kwani walipata tone ya hio dawa iliyokatazwa "metabolites zisizo za asili za testosterone."

Klabu yake ya Juventus ilisema katika taarifa yake kuwa Pogba " aliarifiwa kusimamishwa soka kwa muda kwa tahadhari."

"Klabu ina haki ya kuzingatia hatua zifuatazo za kiutaratibu," taarifa hiyo iliongeza. Ukaguzi wa kimatibabu ilihusisha sampuli "A", Na Pogba anakabiliwa na marufuku ya miaka minne ikiwa vipimo vya sampuli ya "B" pia itatoa matokeo chanya ya testosterone.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Pogba Rafaela Pimenta alisema kwa ujumbe wake ya kuwa, alikuwa " akisubiri sampuli ya pili na hawezi kutoa maoni kabla ya matokeo."

"Cha uhakika ni kwamba Paul Pogba hakutaka kamwe kuvunja sheria," aliongeza.

Pogba aliihamia Juventus mnamo Julai 2022 kutoka Manchester United ya Uingereza.

Kuanzia 2012 hadi 2016 aliisaidia Juventus kushinda mataji manne ya Serie A na Vikombe viwili vya italia, na kuiwezesha kutua fainali ya Ligi ya Mabingwa mnamo 2015.

Pogba alikuwa kiungo muhimu kwenye Ubingwa wa Ufaransa wa Kombe la Dunia 2018, lakini msimu wake wa 2022-23 uliathiriwa na majeraha na sakata ya mamilioni ya euro ya uonevu iliyohusisha marafiki wake wa utotoni na ndugu yake.

Aliiwakilisha Juventus mechi 10 pekee katika msimu huo na hata kutocheza Kombe la Dunia la 2022 na Ufaransa.

Msimu uliopita alishiriki mechi sita za Serie A, lakini alikuwa anatarajiwa kurudi kwenye mechi dhidi ya Lazio mwishoni mwa wiki huku akisema kupitia mahojiano yake na shirika la habari la Al Jazeera kuwa alikuwa alikuwa tayari kurejea.

"Nimepitia mwaka mgumu na hivyo basi niko na hii hasira na hii hamu ya kucheza soka," Pogba aliiambia Al Jazeera. "Watu pekee wanaoweza kukudhuru ni watu walio karibu nawe. Maadui unawajua wako wapi, lakini marafiki, familia, ambao unafikiri wanafurahi ufanisi wako, wanaweza kukuangamiza.

"Lazima uwe mwangalifu, pesa hubadilisha watu, inaweza kuvunja familia," aliyasema juu ya sakata ya ulaghai ya mamilioni ya euro iliyoendeshwa na marafiki wa zamani na kakaye Mattias.

Pogba aliongeza kuwa wakati mwingine alikuwa amevunjwa moyo sana na jambo hilo.

"Nilikuwa peke yangu nikiwaza kuwa sitaki kuwa na pesa tena, sitaki kucheza tena, nataka tu kuwa na watu wa kawaida, ili wanipenda mimi kama mtu, sio kwa umaarufu, sio kwa pesa," alisema.

Baada ya kuvunjwa moyo hivi karibuni Pogba sasa anasubiri kwa matokeo ya uchunguzi wake wa sampuli "B".

AFP