Ujerumani ndio mwenyeji wa EURO 2024 / Picha: AP

Timu za soka za mataifa mbalimbali za bara ulaya zinaingia uwanjani Alhamisi na Ijumaa hii zikilenga kuwa kati ya timu ishirini zitakazotinga moja kwa moja kwenye fainali ya kombe la mataifa bora ulaya zitakazogaragazwa nchini Ujerumani mwaka ujao.

Kufikia sasa, Austria, Ubelgiji, Ufaransa, Ureno, na Scotland ni mojawapo ya timu zenye uwezo wa kujihakikishia nafasi iwapo zitaandikisha matokeo mazuri kwenye mechi za Alhamisi na Ijumaa.

Timu ya Scotland itajihakikishia nafasi iwapo itajiepusha na kulazwa na Uhispania au ikiwa Norway haitashinda.

Nafasi 20 za kwanza zitaamuliwa kupitia hatua za makundi katika mechi za kufuzu, na mbili za juu katika kila sehemu zinaendelea.

Uturuki itachuana na Croatia katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 alhamisi huku ikiwa pia ni mechi ya kwanza ya timu ya taifa ya Uturuki chini ya meneja wake mpya, Vincenzo Montella Wa Italia kwenye kipute dhidi ya Croatia ambao ndio viongozi wa Kundi D.

Montella aliajiriwa mwezi uliopita wa Septemba kumrithi Stefan Kunz aliyeondoka.

Katika mechi nyingine ya kundi D, siku hiyo hiyo, Latvia itakabiliana na Armenia.

Ufaransa itafuzu kutoka kundi B iwapo watakutana na Uholanzi, au iwapo watatoka sare na Ugiriki ipoteze mechi yake dhidi ya Jamhuri ya Ireland.

Aidha, Ureno inahitaji tu ushindi katika mechi yake ya kundi J dhidi ya Slovakia ili kufuzu kutoka kundi la 7.

Kwa jumla, timu 23 zitaungana na wenyeji Ujerumani katika ngarambe ya UEFA EURO 2024 itakayokuwa na timu 24.

Makundi ni kama ifuatavyo:

Kundi A: Uhispania, Scotland, Norway, Georgia, Cyprus

Kundi B: Uholanzi, Ufaransa, Jamhuri ya Ireland, Ugiriki, Gibraltar

Kundi C: ItalIa, Uingereza, Ukraine, Macedonia Kaskazini, Malta

Kundi D: Croatia, Wales, Armenia, Uturuki, Latvia

Kundi E: Poland, Czechia, Albania, Visiwa vya Faroe, Moldova

Kundi F: Ubelgiji, Austria, Sweden, Azerbaijan, Estonia

Kundi G: Hungary, Serbia, Montenegro, Bulgaria, Lithuania

Kundi H: Denmark, Finland, Slovenia, Kazakhstan, Ireland Kaskazini, San Marino

Kundi I: Uswizi, Israel, Romania, Kosovo, Belarus, Andorra

Kundi J: Ureno, Bosnia na Herzegovina, Iceland, Luxembourg, Slovakia, Liechtenstein

Michuano ya UEFA EURO 2024 zitaanza tena tarehe 14/06/2024 kwa mechi ya ufunguzi na kumalizika tarehe 14/07/2024.

TRT Afrika