Mlenga shabaha wa Uturuki Yusuf Dikec amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonesha utulivu wa hali ya juu wakati mchezo wake, na kumuhakikishia medali ya fedha kwenye michezo ya Olimpiki ya 2024.
Picha za mitandaoni zilimuonesha Dikec akiwa amevalia fulana tu huku mkono ukiwa kwenye mfuko wake wa suruali na kuonekana mtu wa kawaida tu, kabla ya kuonesha kiwango cha kushangaza kwenye michuano hiyo.
Hata hivyo, Dikec, sio mgeni kwenye mashindano ya Olimpiki, akiwa ameshiriki toka mwaka 2008.
Baadhi ya picha za utani mitandaoni, zinamuonesha Dikec akiwa na mpinzani wake kutoka Serbia, Damir Mikec, aliyekuwa amefunika jicho moja na vikinga masikio.
Ni kweli Didec alishinda medali?
Ndio, ni kweli na kuingia kwenye vitabu vya historia.
Dikec na Sevval Ilayda Tarhan walishinda medali ya fedha katika timu ya mchanganyiko siku ya Jumanne, na kuihakikishia Uturuki medali ya kwanza kabisa katika mashindano hayo.
Mikec na Zorana Arunovic kutoka Serbia walishinda medali za dhahabu wakati medali za fedha zilienda kwa India, kupitia Manu Bhaker na Sarabjot Singh.
Tofauti na Dikec, mchezaji mwenzake Tarhan alikuwa amevalia kikinga sikio kikuba na kifaa cha kutazamia, akiwa amesuka nywele zenye rangi ya bendera Uturuki. Yeye pia, alitumia mkono mmoja wakati wa kulenga shabaha.
Dikec alishika nafasi ya 13 kwenye michuano hiyo, akijiaandaa michuano ijayo kwa mwaka 2028. “Natumai nitashinda medali ya dhahabu kwenye michezo ijayo itakayofanyika Los Angeles,” alisema siku ya Jumanne.
Anajisikiaje kuwa maarufu ghafla?
Dikec anaonekana kwenda na upepo wa tukio hilo baada ya kuamua kusambaza picha hizo za video kwa lugha ya Kituruki kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Mchezo huo wa kulenga shabaha ulifanyika kusini mwa jiji la Paris.
Dikec na Tarhan walisafiri hadi mji mkuu wa Ufaransa siku ya Jumatano, na kulakiwa kwa shangwe kutoka kwa mashabiki.
Kwanini hakuvaa vifaa zaidi?
Walenga shabaha huwa na uhuru fulani wakati linapokuja suala la mavazi wakati wa mashindano.
Walenga shabaha wengi katika michezo hiyo huchagua kuvaa visura ili kupunguza mng'ao wa taa au kinachojulikana kama vipofu kwenye jicho moja ili kupata umakini zaidi kwa jicho ambalo linatazama chini.
Sio kweli kabisa kwamba Dikec hakuwa amevaa kifaa chochote vya kulenga shabaha. Alikuwa na viunga vya masikioni vya njano kuzuia visumbufu wakati akipiga katika fainali. Hazikuonekana tu katika picha zilisombaa.
Kama ilivyo kwa Dikec, mlenga shabaha wa China Liu Yukun alishinda medali ya dhahabu Alhamisi akiwa amevaa vifunga masikio lakini hakuwa na kizuia macho.
Je, walenga shabaha wamepata umaarufu kama huo?
Ndio, Kim Yeji's kutoka Korea Kusini amesifika kutokana kwa kujiamini kwake.
Kim alishinda medali ya fedha siku ya Jumapili, akifuatiwa na mwenzake Oh Ye Jin. .
Kim anatazamiwa kushindana tena siku ya Ijumaa katika kufuzu kwa mashindano ya kulenga shabaha ya mita 25 kwa upande wa wanawake.