Kipa wa Cameroon na Manchester United Andre Onana amerejea timu ya taifa kwa mechi za kimataifa kwa kukubali mwaliko wa ghafla wa 'Indomitable Lions' kwa ajili ya mechi yao ijayo ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies dhidi ya Burundi mnamo Septemba 12.
Onana amerejea ghafla miezi minane tu baada ya kukaribishwa tena kikosini na kocha Song.
"Hamu yangu ya kuwakilisha nchi yangu haijawahi kuyumba tangu ujana wangu, na matarajio haya yanasalia kuwa sehemu isiyoweza kutenganishwa ya utambulisho wangu. Ninajibu wito wa taifa langu kwa uhakika usiotikisika, nikifahamu kwamba kurudi kwangu si tu kuheshimu ndoto yangu, bali pia kujibu matarajio na uungwaji mkono wa Wacameroon, ambao wanastahili timu ya taifa iliyodhamiria kung'ara.
Golikipa huyo alistaafu kwa hasira akiwa na umri wa miaka 26 tu lakini licha ya hayo, kila mara alidumisha upendo wake wa "milele" kwa timu ya taifa.
Kurejea kwa Onana miezi minane tu baada ya kuondoka kwa kombe la dunia kwa mbwembwe kulionekana kuhitimisha soka yake ya kimataifa kabla ya wakati wake, lakini sasa ana nafasi ya kuzidisha idadi ya mechi zake 34 alizoichezea Cameroon.
Hata hivyo kurejea kwa Andre Onana Cameroon ni pigo kwa United kwani huenda akakosa hadi mechi saba za Manchester United wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON litakaloanza Januari 13 kwa mechi ya ufunguzi kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Ebimpe, Abidjan hadi 11 Februari.
Mechi ambazo Ande Onana atazikosa ni :
- 8 Januari 2024 Carabao Cup nusu-fainali ya kwanza
- 13 Januari 2024 Premier League Man Utd vs Tottenham
- 22 January 2024 Carabao Cup nusu-fainali ya pili
- 27 Januari 2024 kombe la FA CUP raundi ya 4
- 30 Januari 2024 Premier League Wolves vs Man Utd
- 3 Februari 2024 Premier League Man Utd vs West Ham
- 10 Februari 2024 Premier League Aston Villa vs Man Utd
- 17 Februari 2024 Premier League Luton vs Man Utd
Cameroon inahitaji sare pekee dhidi ya Burundi ikiwa nyumbani baadaye mwezi huu ili kujipatia nafasi ya kufuzu kwa fainali za AFCON 2023.