Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wakiwa wanalaumiana kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur./Picha: Getty

Manchester United ya Uingereza imeendelea na mwenendo mbaya kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kufungwa mabao 3-0 na Tottenham Hotspur kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mabao ya Brennan Johnson, Dejan Kulusevski na Dominic Solanke yalitosha kabisa kuharibu wikiendi ya vijana wa Erik ten Hag ambao pia walimaliza wakiwa pungufu baada ya Bruno Fernandes kuoneshwa kadi nyekundu, kwenye mchezo huo uliofanyika Septemba 29. 2024.

Wachezaji wa Tottenham Hotspur wakishangilia ushindi dhidi ya Manchester United./Picha: Getty

Matokeo hayo yanaweza kuweka kibarua cha Erik Teg Hag rehani, haswa baada ya kuponea chupu chupu kwenye msimu wa joto.

Manchester United iko nafasi ya 12 ikiwa na alama 7 baada ya michezo 6 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

'Mashetani hao Wekundu' wameshinda michezo miwili, kutoka sare mchezo mmoja na kupoteza michezo mitatu kwenye ligi hiyo.

TRT Afrika