#LBL28 : Football: Premier League - day 36 / Photo: AFP

Nyota wawili wa zamani Paul Scholes na Michael Owen, walikuwa wakizungumza baada ya Manchester United kufungwa 4-0 na Crystal Palace.

Kwa upande wake, Meneja wa Manchester United Erik Ten Hag amesisitiza kuwa bado ndiye Kocha anayefaa kufufua klabu hiyo.

Nimekaa hapa kwa muda mrefu na nimekuwa nikisema kwamba Ten Hag sio mtu sahihi kwa kazi hii. Nimesema mara kwa mara, hawezi, hawezi tu, kusimamia timu msimu ujao.

Michael Owen

Ten Hag amekuwa na msimu mbaya na Red Devils ikiwa katika nafasi ya nane katika meza, mbali na kusubiriwa na fainali ngumu ya Kombe la FA ambapo watakuwa wakikabiliana na wapinzani wao wa karibu Manchester City.

Kwa mara ya kwanza Crystal Palace iliifunga United kwenye ligi mara mbili juu ya United kupitia mabao mawili ya Michael Olise, goli la Jean-Philippe Mateta na Tyrick Mitchell kuifunga United kwa mechi yake ya 18, ikiwa ni ya juu zaidi katika msimu tangu 1977-78.

Aidha, Ushindi wa Palace dhidi ya United umewapa Red Devils kipigo chao cha 13 katika Ligi kuu msimu huu, ikiwa mechi nyingi zaidi walizopoteza kwenye ligi katika historia yao ya miaka 32 kwenye Ligi.

Huenda United ikamaliza nje ya timu saba bora kwa mara ya kwanza tangu 1990.

AFP