Diego Forlán nyota wa zamani wa soka ajaribu bahati yake kwenye mchezo wa tenisi

Diego Forlán nyota wa zamani wa soka ajaribu bahati yake kwenye mchezo wa tenisi

Diego Forlán amewahi kucheza katika klabu maarufu  ikiwemo Manchester United, Atletico Madrid na Intermilan.
Diego Forlán amehamia mchezo wa tenisi, baada ya kustaafu kama mchezaji wa soka. /Picha: Reuters

Maisha mapya ya nyota wa zamani wa soka, Diego Forlán, yameanza katika taaluma ya tenisi kwa kushindwa mara mbili kwenye michuano ya Uruguay Open, uliochezwa siku ya Jumatano.

Forlán, mwenye umri wa miaka 45, alicheza pamoja na Federico Coria kutoka Argentina lakini walishindwa 6-1, 6-2 na Boris Arias pamoja na Federico Zeballos katika raundi ya kwanza ya ATP Challenger Tour, michuano ya daraja la pili.

Mshambuliaji huyo wa Uruguay alistaafu soka mwaka 2019 baada ya kufanikiwa kucheza katika klabu maarufu kama Manchester United, Atletico Madrid na Inter Milan.

Forlán alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia mwaka 2010, na mwaka uliofuata, alifunga mara mbili katika fainali ya Copa America 2011, akiiwezesha Uruguay kutwaa taji lake la kwanza la bara baada ya miaka 16.

Diego Forlán alistaafu soka mwaka 2019 baada ya kufanikiwa kucheza katika klabu maarufu kama Manchester United, Atletico Madrid na Inter Milan. /Picha: Reuters
AP